Hakika Mwenyezi Mungu humpenda mja mchamungu, mwenye kutosheka, mnyenyekevu
Wema, Uadilifu na Tabia Njema
Kiarabu
عن سعد بن أبي وقاص رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «إِنَّ اللهَ يُحِبُّ الْعَبْدَ التَّقِيَّ الْغَنِيَّ الْخَفِيَّ».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokewa kutoka kwa Sa'd bin Abii Waqas -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika Mwenyezi Mungu humpenda mja mchamungu, mwenye kutosheka, mnyenyekevu".
English translation
Sa‘d ibn Abi Waqqās (may Allah be pleased with him) reported: I heard the Messenger of Allah (may Allah’s peace and blessings be upon him) say: "Verily, Allah loves the servant who is pious, free of wants, and inconspicuous."
Maelezo
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anawapenda baadhi ya waja wake, Na miongoni mwao ni mchamungu: Mwenye kutekeleza amri za Allah, mwenye kuyaepuka makatazo yake. Na anampenda mwenye kutosheka: Aliyetosheka kutowahitajia watu kwa kumuelekea Mwenyezi Mungu Mtukufu wala hageuki kwa mwingine. Na anampenda mnyenyekevu: Mwenye kujinyenyekeza, mwenye kumuabudu Mola wake Mlezi, mwenye kujishughulisha na yenye kumnufaisha, ambaye hashughuliki na kutaka yeyote amjue au amzungumze kwa sifa au shukurani.
Faida
- Zimebainishwa baadhi ya sifa zinazopelekea mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, nazo ni uchamungu na unyenyekevu na kuridhika na yale aliyoyagawa Mwenyezi Mungu.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.