Atakayeitetea heshima ya ndugu yake basi Mwenyezi Mungu ataukinga uso wake na moto siku ya Kiyama
Wema, Uadilifu na Tabia Njema
Kiarabu
عن أبي الدرداء رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ رَدَّ عَنْ عِرْضِ أَخِيهِ رَدَّ اللهُ عَنْ وَجْهِهِ النَّارَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokewa kutoka kwa Abuu Dardaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayeitetea heshima ya ndugu yake basi Mwenyezi Mungu ataukinga uso wake na moto siku ya Kiyama".
English translation
Abu ad-Dardā’ (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (may Allah’s peace and blessings be upon him) said: "Whoever protects the honor of his brother in his absence, Allah will protect his face from the Fire on the Day of Judgment."
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeitetea heshima ya ndugu yake muislamu akiwa hayupo (katika mazungumzo) kwa kukataza watu kumsema vibaya na kumkosea adabu, basi naye Mwenyezi Mungu ataizuia adhabu kwake siku ya Kiyama.
Faida
- Katazo la kuzungumza kuhusu heshima za waislamu.
- Malipo huendana na matendo, atakayeirudisha heshima ya ndugu yake Mwenyezi Mungu naye atauzuia moto kwake.
- Uislamu ni dini ya udugu na kuteteana kati ya waislamu.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.