Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sunan Ibn Majah · Na. HE-5499

Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye haya Mkarimu, anamuonea haya mja wake atakapo nyanyua mikono yake kumuelekezea kisha amrejeshe patupu

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ سَلْمَانَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ رَبَّكُمْ حَيِيٌّ كَرِيمٌ، يَسْتَحْيِي مِنْ عَبْدِهِ إِذَا رَفَعَ يَدَيْهِ إِلَيْهِ أَنْ يَرُدَّهُمَا صِفْرًا».

Tafsiri ya Kiswahili

Na kutoka kwa Salmani -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye haya Mkarimu, anamuonea haya mja wake atakapo nyanyua mikono yake kumuelekezea kisha amrejeshe patupu".

English translation

Salmān (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Verily, your Lord is Bashful and Munificent. He is too Bashful of His slave to let him go empty-handed when raising his hands to Him."

Maelezo

Anahimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kunyanyua mikono wakati wa dua, na akaeleza kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu "huona haya" mwingi wa haya, na haachi kutoa, anamfanyia mja yenye kumfurahisha, na anaacha yenye kumdhuru, "Ni Mkarim" hutoa pasina kuombwa, je hali huwaje baada ya kuombwa! anamuonea haya mja wake muumini kuirejesha patupu mikono yake baada ya kuinyanyua kwa ajili ya dua ikiwa imefeli haina kitu kwa kutojibiwa.

Faida

  • Kila anapodhihirisha mwanadamu unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumuabudu, ndivyo inavyotarajiwa kwake kuwa na ukaribu wa kujibiwa.
  • Himizo la kuomba dua, na kupendeza kunyanyua mikono ndani yake, nakuwa kufanya hivyo ni katika sababu za kujibiwa.
  • Kumebainishwa upana wa ukarimu wa Mwenyezi Mungu na rehema yake kwa waja wake .

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)