Hakika watoa laana hawatokuwa mashahidi wala watetezi siku ya Kiyama
Wema, Uadilifu na Tabia Njema
Kiarabu
عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ رضي الله عنه: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «إِنَّ اللَّعَّانِينَ لَا يَكُونُونَ شُهَدَاءَ وَلَا شُفَعَاءَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa kutoka kwa Abud-dardaa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hakika watoa laana hawatokuwa mashahidi wala watetezi siku ya Kiyama".
English translation
Abu ad-Dardā’ (may Allah be pleased with him) reported: I heard the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) say: "Indeed, the cursers will not be witnesses or intercessors on the Day of Judgment."
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye kukithirisha laana kwa mtu asiyestahiki huyu anastahiki kupata adhabu mbili. Ya kwanza: Hatokuwa shahidi siku ya Kiyama juu ya umma kwa mitume wao kufikisha ujumbe kwao, na wala haukubaliki ushahidi wake duniani; kwa sababu ya uovu wake, na wala hatoruzukiwa shahada, nako ni kufa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Ya pili: Hatopewa nafasi ya kutoa utetezi siku ya Kiyama wakati ambapo waumini wataomba utetezi kwa ndugu zao waliostahiki moto.
Faida
- Uharamu wa kutoa laana, nakuwa kukithirisha hilo ni dhambi miongoni mwa madhambi makubwa.
- Adhabu iliyotajwa katika hadithi inamuhusu anayekithirisha kulaani, si wa mara moja na mfano wake, kwa sababu kwake pia kunatoka laana za halali, nazo ni zile ambazo sheria imekuja kuwalaani watu wenye sifa mbaya pasina kumuainisha mtu, kama kusema: "Mwenyezi Mungu awalaani Mayahudi na Wakristo", "Laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya madhalimu" Mwenyezi Mungu amewalaani wanaopiga picha", "Mwenyezi Mungu amemlaani atakayefanya vitendo vya watu wa Luti", "Mwenyezi Mungu amemlaani atakayechinja kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu", "Mwenyezi Mungu amewalaani wanaume wenye kujifananisha na wanawake, na wanawake wenye kujifananisha na wanaume", na mfano wa hizo.
- Kumethibitishwa uombezi wa waumini siku ya Kiyama.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.