Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih Muslim · Na. HE-5474

Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgomvi mkorofi

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عن عائشة رضي الله عنها عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «إِنَّ أَبْغَضَ الرِّجَالِ إِلَى اللهِ الْأَلَدُّ الْخَصِمُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgomvi mkorofi".

English translation

‘Ā’ishah (may Allah be pleased with her) reported: The Prophet (may Allah’s peace and blessings be upon him) said: "The most hated person in the sight of Allah is the most quarrelsome person."

Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- anawachukia miongoni mwa watu mwenye ugomvi mkali na mwingi, asiyekubali kutii haki, na anajaribu kuikataa kwa mijadala, au akagombana kwa haki akapitiliza katika ugomvi na akatoka katika mpaka wa uadilifu, na akajadiliana bila elimu.

Faida

  • Haingii katika mlango wa mgomvi mbaya, aliyedhulumiwa kudai haki yake kwa njia ya kushitakiana kisheria.
  • Mijadala na ugomvi ni katika maafa ya ulimi yanayosababisha kutengana na kupeana migongo kati ya waislamu.
  • Mjadala ni mzuri utapokuwa katika haki na utaratibu mzuri, na unakuwa mbaya utapokuwa ni kwa kuikataa haki na kuitetea batili, au ukawa bila hoja wala ushahidi.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)