Atakayekwenda asubuhi msikitini au mchana, Mwenyezi Mungu humuandalia nyumba peponi kila anapotoka asubuhi au jioni
Hukumu za Swala na Tohara
Kiarabu
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ غَدَا إِلَى الْمَسْجِدِ أَوْ رَاحَ أَعَدَّ اللهُ لَهُ فِي الْجَنَّةِ نُزُلًا، كُلَّمَا غَدَا أَوْ رَاحَ».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayekwenda asubuhi msikitini au mchana, Mwenyezi Mungu humuandalia nyumba peponi kila anapotoka asubuhi au jioni"
English translation
Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Whoever goes to the mosque in the morning or the evening, Allah has prepared an abode for him in Paradise every time he goes in the morning or the evening."
Maelezo
Amempa habari njema Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kwenda msikitini kwa ajili ya ibada au elimu kwa lengo jingine katika mambo ya kheri katika wakati wowote; mwanzo wa mchana au mwisho wake kuwa Mwenyezi Mungu amemuandalia mahali na takrima ya ugeni peponi, kila anapokuja msikitini usiku au mchana.
Faida
- Fadhila za kwenda msikitini, na himizo la kuhifadhi swala ya jamaa ndani ya msikiti, kwani anapitwa na daraja ngapi mwenye kukwepa kwenda msikitini na kheri na fadhila na malipo na ugeni aliouandaa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa mwenye kwenda katika nyumba yake.
- Ikiwa watu humkirimu anayewajia katika majumba yao, na kumletea chakula, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mkarimu zaidi kuliko viumbe wake! Yeyote atakayekwenda katika nyumba yake basi atamkirimu, na Mwenyezi Mungu atamuandalia mafikio ya thamani na yenye nafasi kubwa.
- Furaha na moyo mkunjufu wakati wa kwenda msikitini; kwa sababu anaandaliwa makazi kila anapokwenda asubuhi au mchana kwa idadi ya kwenda kwake.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.