Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu, kisha akaja katika swala ya Ijumaa akasikiliza na akanyamaza atasamehewa yale yaliyoko kati ya Ijumaa yake hiyo na Ijumaa ijayo na ziada ya siku tatu
Hukumu za Swala na Tohara
Kiarabu
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ تَوَضَّأَ فَأَحْسَنَ الْوُضُوءَ ثُمَّ أَتَى الْجُمُعَةَ فَاسْتَمَعَ وَأَنْصَتَ غُفِرَ لَهُ مَا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الْجُمُعَةِ وَزِيَادَةُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ، وَمَنْ مَسَّ الْحَصَى فَقَدْ لَغَا».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu, kisha akaja katika swala ya Ijumaa akasikiliza na akanyamaza atasamehewa yale yaliyoko kati ya Ijumaa yake hiyo na Ijumaa ijayo na ziada ya siku tatu, na atakayegusa kijiwe basi atakuwa kafanya mchezo"
English translation
Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "He who performs ablution properly and then comes to the Friday prayer and listens to it attentively and keeps silent, his sins between that Friday and the following Friday will be forgiven, with the addition of three more days; but he who touches a pebble has engaged in idle activity."
Maelezo
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye kutawadha na akaufanya vyema udhu wake kwa kukamilisha nguzo zake na kufuata Sunna zake na adabu zake, kisha akaswali swala ya Ijumaa na akanyamaza na kumsikiliza mhutubu, na akanyamaza pasina kuleta mazungumzo yasiyofaa; Basi Mwenyezi Mungu atamsamehe madhambi yake madogo kwa muda wa siku kumi, kuanzia sala ya Ijumaa hadi Ijumaa ya pili na ziada ya siku tatu, kwa sababu jambo jema huzidishwa mara kumi. Kisha rehema na amani ziwe juu yake akatahadharisha juu ya moyo kutojali mawaidha yanayosemwa katika hotuba, na kuchezea viungo kwa kugusa kokoto na aina nyinginezo za upuuzi na kujishughulisha, hayo yote ni katika aina ya mchezo na kujishughulisha kusikofaa, kwani mwenye kufanya hivyo atakuwa kafanya mchezo, na atakayefanya mchezo atakuwa hana fungu kamili katika ujira wa swala ya Ijumaa.
Faida
- Himizo la kutawadha na kuukamilisha kikamilifu, na kushikamana na sala ya Ijumaa.
- Fadhila za swala ya Ijumaa.
- Ulazima wa kunyamaza kwa ajili ya hotuba ya Ijumaa, na kutojishughulisha kwa mazungumza au kinginecho.
- Iwapo mtu atafanya mchezo wakati wa hotuba Swala ya Ijumaa itakuwa sahihi na haitomlazimu kurudia swala ya faradhi, isipokuwa itakuwa na upungufu wa malipo.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.