Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sahih Muslim · Na. HE-5378

Hana swala yeyote ambaye hakusoma sura kifunguzi cha kitabu (suratul faatiha)

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا صَلَاةَ لِمَنْ لَمْ يَقْرَأْ بِفَاتِحَةِ الكِتَابِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Ubaada bin Swaamit -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume -Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Hana swala yeyote ambaye hakusoma sura kifunguzi cha kitabu (suratul faatiha)".

English translation

‘Ubādah ibn as-Sāmit (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "The prayer of the one who did not recite the Opening of the Book (Surat al-Fātihah) is invalid."

Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa sala haikubaliki isipokuwa kwa kusoma suratul Fatiha, nayo ni nguzo miongoni mwa nguzo za swala, katika kila rakaa.

Faida

  • Haikubaliki kusoma sura isiyokuwa suratul Fatiha ikiwa ana uwezo wa kuisoma.
  • Kuharibika kwa rakaa ambayo haikusomwa ndani yake suratul fatiha, kwa mwenye kufanya kusudi na mjinga na aliyesahau; kwa sababu ni nguzo, na nguzo huwa hazidondoki kwa hali yoyote ile.
  • Kisoma cha Suratul Fatiha kinaondoka kwa maamuma anapomkuta imam karukuu.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)