Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Sunan Abu Dawud · Na. 4031

Atakaye jifananisha na watu fulani basi na yeye ni miongoni mwao

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عن ابنِ عُمَرَ رضي الله عنهما قال: قال رسولُ الله صلَّى الله عليه وسلم: «مَن تَشَبَّهَ بِقَوْمٍ فَهُوَ مِنْهُمْ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakaye jifananisha na watu fulani basi na yeye ni miongoni mwao".

English translation

Ibn ‘Umar (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Whoever imitates a people is one of them."

Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakaye jifananisha na watu fulani katika makafiri au waovu au wema -na hii ni pale atakapofanya jambo katika mambo yao mahususi, kama itikadi au ibada au tamaduni basi naye ni miongoni mwao-; kwa sababu kujifananisha nao katika muonekano kunapelekea kujifananisha nao kiundani, na hakuna shaka kuwa kujifananisha na watu fulani kunasababishwa na kupendezwa nao, na huenda kukapelekea kuwapenda na kuwatukuza na kuwategemea, na hili huenda likampelekea mtu hata kujifananisha kiundani na katika ibada -Tunamuomba Allah atukinge na hilo-.

Faida

  • Tahadhari ya kujifananisha na makafiri na waovu.
  • Himizo la kujifananisha na watu wema na kuiga kutoka kwao.
  • Kujifananisha katika muonekano hutia mapenzi katika moyo.
  • Mtu hupata kemeo la adhabu na madhambi kulingana na namna ya kujifananisha na aina yake.
  • Katazo la kujifananisha na makafiri katika dini yao na katika desturi zao mahususi kwao, ama yasiyokuwa hayo kama kujifunza ufundi na mfano wake hayaingii katika katazo.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)