Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih Muslim · Na. 2626

Kamwe!, Usidharau chochote katika wema, hata kama ni kukutana na ndugu ukiwa na uso mkunjufu

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عن أبي ذر رضي الله عنه قال: قال لي النبي صلى الله عليه وسلم: «لَا تَحْقِرَنَّ مِنَ الْمَعْرُوفِ شَيْئًا، وَلَوْ أَنْ تَلْقَى أَخَاكَ بِوَجْهٍ طَلْقٍ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abuu Dhari -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alisema kuniambia mimi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kamwe!, Usidharau chochote katika wema, hata kama ni kukutana na ndugu ukiwa na uso mkunjufu".

English translation

Abu Dharr (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said to me: "Do not belittle any good deed, even if it be meeting your brother with a cheerful face."

Maelezo

Amehimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya kutenda wema, na mtu asiudharau hata kama utakuwa kidogo, na miongoni mwake ni ukunjufu wa uso kwa kutabasamu wakati wa kukutana, ni lazima kwa muislamu alipupie hilo; kwa sababu hujenga kuwa na ukaribu na ndugu yako muislamu na huingiza furaha kwake.

Faida

  • Fadhila za kupendana kati ya waumini, na kutabasamu na bashasha wakati wa kukutana.
  • Ukamilifu wa sheria hii na kugusa kwake kila sekta, nakuwa imekuja na mambo yote ambayo yana masilahi kwa waislamu na kuunganisha umoja wao.
  • Himizo la kutenda wema hata kama ni kidogo.
  • Inapendeza kuingiza furaha kwa waislamu; kwani ndani yake kuna kuleta ukaribu baina yao.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)