Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih Muslim · Na. 2563

Tahadharini na dhana; kwani dhana ni mazungumzo ya uongo mno

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: «إِيَّاكُمْ وَالظَّنَّ؛ فَإِنَّ الظَّنَّ أَكْذَبُ الْحَدِيثِ، وَلَا تَحَسَّسُوا، وَلَا تَجَسَّسُوا، وَلَا تَحَاسَدُوا، وَلَا تَدَابَرُوا، وَلَا تَبَاغَضُوا، وَكُونُوا عِبَادَ اللهِ إِخْوَانًا».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Tahadharini na dhana; kwani dhana ni mazungumzo ya uongo mno, na wala msitiliane shaka (kwa kuhisiana vibaya), na wala msichunguzane, na wala msihusudiane, na wala msitengane, na wala msichukiane, na kuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu wamoja"

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Beware of false thought, for false thought is the most untruth speech. Do not search for the faults of one another, do not spy on one another, do not envy one another, do not turn your backs on one another, do not harbor hatred for one another, and be, O slaves of Allah, brothers."

Maelezo

Anakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na anatahadharisha baadhi ya yale yanayoweza kupelekea kufarakana na uadui baina ya waislamu, na miongoni mwayo: (Dhana) Nazo ni tuhuma zinazojitokeza ndani ya moyo pasina ushahidi, na akabainisha kuwa hayo ni mazungumzo ya uongo mno. Na kuhusu (kuhisiana vibaya): Nako ni kutafuta aibu za watu kwa kutazama au kusikiliza. (Na kupelelezana): Nako ni kutafuta yaliyofichikana miongoni mwa mambo, na hii hutumika zaidi katika shari. Na kuhusu: (Husuda) nako ni kuchukia kupatikana kwa neema kwa watu wengine. Na kuhusu (Kutengana) kwa kuwapuuza baadhi ya watu wenzao, hamsalimii wala hamtembelei ndugu yake muislamu, Na kuhusu: (Kuchukiana) na kuchukia na kubeza, kama kuwaudhi watu wengine, na kutotabasamu, na kukutana nao kwa sura mbaya. Kisha akazungumza neno moja linalokusanya kila kitu, ambalo litatengeneza hali za waislamu baadhi yao kwa baadhi: (Na kuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu wamoja). Udugu ni kiunganishi kinachounganisha mahusiano kati ya watu, na kinazidisha mapenzi na kuzoeana baina yao.

Faida

  • Dhana mbaya haidhuru kwa mtu ambaye zimedhihiri kwake alama zake, na ni wajibu juu ya muumini awe mwerevu mjanja, hadanganyiki na watu waovu na mafasiki.
  • Makusudio yake ni kutahadharisha na tuhuma ambazo zinabakia ndani ya nafsi, na kuziendeleza, ama yanayojitokeza ndani ya nafsi na hayabakii haya mtu hachukuliwi katenda dhambi.
  • Kuchukua tahadhari dhidi ya sababu za kubezana na kukata mahusiano baina ya jamii ya kiislamu, ikiwemo ujasusi na husuda na mfano wake.
  • Usia kwa muislamu wa kuamiliana na ndugu yake muamala wa ndugu kwa ndugu katika nasaha na mapenzi.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)