Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 3118

Hakika watu wanaotumia mali ya Mwenyezi Mungu pasina haki, hao (wana adhabu ya) moto siku ya Kiyama

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عن خَولة الأنصاريةِ رضي الله عنها قالت: سمعت النبي صلى الله عليه وسلم يقول: «إِنَّ رِجَالًا يَتَخَوَّضُونَ فِي مَالِ اللهِ بِغَيْرِ حَقٍّ، فَلَهُمُ النَّارُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Khaula Al-Answariya -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika watu wanaotumia mali ya Mwenyezi Mungu pasina haki, hao (wana adhabu ya) moto siku ya Kiyama".

English translation

Khawlah al-Ansāriyyah (may Allah be pleased with her) reported: I heard the Messenger of Allah (may Allah’s peace and blessings be upon him) say: "Some people dispose of Allah's property wrongfully. For them will be Hellfire on the Day of Judgment."

Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu watu wanaotumia mali ya waislamu kwa batili, na wanaichukua pasina haki, na maana hii inajumuisha kuanzia ukusanyaji wake, na uchumaji wake bila uhalali wake, na utoaji wake katika sehemu zisizo sahihi, na inaingia katika hilo kula mali ya yatima na mali ya wakfu, na kutotunza amana, na kuchukua chochote katika mali ya umma bila ya haki. Ameeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa malipo yao ni moto siku ya Kiyama.

Faida

  • Mali iliyoko mikononi mwa watu ni mali ya Mwenyezi Mungu, amewamilikisha ili waitoe katika njia za kisheria, na waepuke kuitumia katika batili, na hii inawahusu viongozi na wasiokuwa viongozi.
  • Sheria imetia mkazo katika mali ya umma, nakuwa yeyote atakayesimamia chochote basi atambue kuwa atahesabiwa juu ya ukusanyaji wake na matumizi yake.
  • Anaingia katika ahadi hii ya adhabu mwenye kufanya matumizi yasiyokuwa ya kisheria katika mali, sawa sawa iwe ni mali yake, au mali ya mwingine.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)