Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih Muslim · Na. HE-5280

Atakapopiga mwayo mmoja wenu basi na ashike mkono wake juu ya kinywa chake, kwani Shetani huingia

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَن أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِذَا تَثَاءَبَ أَحَدُكُمْ فَلْيُمْسِكْ بِيَدِهِ عَلَى فِيهِ، فَإِنَّ الشَّيْطَانَ يَدْخُلُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapopiga mwayo mmoja wenu basi na ashike mkono wake juu ya kinywa chake, kwani Shetani huingia".

English translation

Abu Sa‘īd al-Khudri (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "When any of you yawns, let him put his hand over his mouth, for indeed, the devil enters."

Maelezo

Amemuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kupiga mwayo pale alipofungua kinywa chake kwa sababu ya uvivu au kujaa na mfano wake; kuwa aweke mkono wake juu ya kinywa chake ili akifunge kwa mkono; na hii ni kwa sababu Shetani huingia ndani yake anapokiacha wazi, kuweka mkono kunakuwa ni kizuizi cha kumzuia kuingia.

Faida

  • Atakapotaka mtu kupiga miayo anatakiwa auzuie kwa kadiri awezavyo, kwa kuuzuia mdomo wake, na aubakishe ukiwa umefungwa wala usifunguke, asipoweza kuubakisha mdomo wake ukiwa umefungwa basi aweke mkono wake juu ya mdomo wake, afunike kinywa chake kwa mkono wake.
  • Kushikamana na adabu za kiislamu katika hali zote; kwa sababu ndio anwani ya ukamilifu na tabia njema.
  • Kuchukua tahadhari ya kila mapitio ya Shetani kwa mwanadamu.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)