Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Musnad Ahmad · Na. HE-4964

Kikoi cha muislamu kifikie nusu ya muundi, na wala hakuna tabu wala hakuna ubaya kikiwa kati yake na kati ya fundo mbili za miguu, kitakachokuwa chini ya fundo mbili basi hicho ni motoni, na atakayeburuza kikoi chake kwa kiburi hatomtazama Mwenyezi Mungu

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ أبي سَعيدٍ الخُدريَّ رضي الله عنه قال: قال رسولُ الله صلَّى الله عليه وسلم ِ: «إزْرَةُ المُسْلمِ إلى نصفِ السَّاق، وَلَا حَرَجَ -أو لا جُنَاحَ- فيما بينَهُ وبينَ الكعبينِ، وما كان أسفلَ منَ الكعبين فهو في النار، مَن جرَّ إزارَهُ بطرًا لم يَنْظُرِ اللهُ إليه».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Kikoi cha muislamu kifikie nusu ya muundi, na wala hakuna tabu wala hakuna ubaya kikiwa kati yake na kati ya fundo mbili za miguu, kitakachokuwa chini ya fundo mbili basi hicho ni motoni, na atakayeburuza kikoi chake kwa kiburi hatomtazama Mwenyezi Mungu".

English translation

Abu Sa‘īd al-Khudri (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "The Muslim's lower garment should be halfway down the leg. There is no harm - or there is no blame - between that and the ankles. However, what is below the ankles is in the Fire. Whoever trails his lower garment out of vanity, Allah will not look at him."

Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwanaume muislamu katika kikoi chake, nacho ni kila kinachositiri nusu ya chini kwa wanaume, kwa hali tatu: Ya kwanza: Inayopendeza iwe kati kati ya muundi. Ya pili: Inayojuzu pasina karaha ni ile inayokuwa chini ya kongo mbili; nayo ni mifupa miwili iliyotokeza katika maungio ya muundi na mguu. Ya tatu: Iliyoharamishwa, nayo ni ile inayokuwa chini ya kongo mbili, na inahofiwa kwake kupatwa na adhabu ya moto, na ikiwa ni kwa kiburi na kwa kufurahia na ujeuri, Mwenyezi Mungu hatomtazama.

Faida

  • Sifa hii na ahadi hii ya adhabu ni maalumu kwa wanaume, ama wanawake, wanaondolewa katika hilo; kwa sababu wao wameamrishwa kusitiri mwili wao wote.
  • Kila kinachositiri nusu ya chini kwa wanaume huitwa kikoi; kama suruali, na nguo na vinginevyo, na vyote hivyo vinaingia katika hukumu ya kisheria iliyotajwa katika hadithi.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)