Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih Muslim · Na. 1048

Lau mwanadamu angelikuwa na mabonde mawili ya mali basi angelitafuta la tatu

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ أَنَسٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَوْ كَانَ لِابْنِ آدَمَ وَادِيَانِ مِنْ مَالٍ لَابْتَغَى وَادِيًا ثَالِثًا، وَلَا يَمْلَأُ جَوْفَ ابْنِ آدَمَ إِلَّا التُّرَابُ، وَيَتُوبُ اللهُ عَلَى مَنْ تَابَ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Anas -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Lau mwanadamu angelikuwa na mabonde mawili ya mali basi angelitafuta la tatu, na hakuna kinachoweza kujaza tumbo la mwanadamu isipokuwa udongo, na Mwenyezi Mungu humsaheme mwenye kuomba msamaha".

English translation

Anas (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "If the son of Adam were to possess two valleys full of wealth, he would seek the third. Nothing can fill his belly except dust, and Allah accepts the repentance of whoever repents."

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba lau kama mwanadamu angelipata bonde moja lililojaa dhahabu, basi angependa kwa sababu ya tamaa yake ambayo ndiyo maumbile yake awe na mabonde mengine mawili, na kwamba mwanadamu haachi kuipupia dunia mpaka anakufa na lijae tumbo lake kwa udongo wa kaburi lake.

Faida

  • Pupa kubwa ya mwanadamu ya kukusanya mali na vinginevyo katika starehe za Dunia.
  • Amesema Nawawi: Hapa kumekemewa pupa ya kuipupia Dunia na kupenda wingi wa mali na kuwa na tamaa.
  • Mwenyezi Mungu anaikubali toba ya mwenye kutubia kutokana na sifa mbaya.
  • Amesema Nawawi: Hadithi imekuja katika mfumo wa kueleza hali ya wanadamu wengi katika kuipupia Dunia, na inaungwa mkono na kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Na Mwenyezi Mungu humsamehe mwenye kuomba msamaha".

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)