Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih Muslim · Na. 1827

Hakika waadilifu mbele ya Mwenyezi Mungu watakuwa katika mimbari za nuru, kuliani mwa Allah Mtukufu, na mikono yake yote miwili ni kulia

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «إِنَّ الْمُقْسِطِينَ عِنْدَ اللهِ عَلَى مَنَابِرَ مِنْ نُورٍ، عَنْ يَمِينِ الرَّحْمَنِ عَزَّ وَجَلَّ، وَكِلْتَا يَدَيْهِ يَمِينٌ، الَّذِينَ يَعْدِلُونَ فِي حُكْمِهِمْ وَأَهْلِيهِمْ وَمَا وَلُوا».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa kutoka kwa Abdullahi bin Amry -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika waadilifu mbele ya Mwenyezi Mungu watakuwa katika mimbari za nuru, kuliani mwa Allah Mtukufu, na mikono yake yote miwili ni kulia , wale wanaofanya uadilifu katika hukumu zao na familia zao, na vile wanavyovitawala"

English translation

‘Abdullāh ibn ‘Amr (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah’s peace and blessings be upon him) said: "Those who act justly will be with Allah on pulpits of light at the right Hand of the Most Compassionate, Exalted be He, and both His Hands are right. They are those who are just in their judgment and towards their people and what is under their charge."

Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa wanaohukumu kwa uadilifu na haki baina ya watu walio chini ya utawala wao na hukumu zao, na familia zao, nikuwa watakaa katika makao ya juu zaidi yaliyoumbwa kwa nuru, ikiwa ni takrima kwao siku ya Kiyama. Na mimbari hizi ziko kuliani mwa Allah Mtukufu, na mikono yake miwili Mtukufu yote ni kulia.

Faida

  • Fadhila za uadilifu na himizo juu yake.
  • Uadilifu ni neno la kiujumla linalokusanya tawala zote, na hukumu za kati ya watu hata uadilifu kati ya wake na watoto, na mengineyo.
  • Kumebainishwa nafasi ya waadilifu siku ya Kiyama.
  • Kutofautiana kwa makazi ya watu wa imani siku Kiyama kila mmoja atakuwa kulingana na matendo yake.
  • Mfumo wa kuhamasisha ni katika njia za kufanya da'wa zinazomvutia mwenye kulinganiwa kuja katika utiifu.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)