Nyuma

Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu (madhambi ya) kukosea na kusahau, na yale waliyolazimishwa

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إنَّ اللَّهَ تَجَاوَزَ لِي عَنْ أُمَّتِي الخَطَأَ وَالنِّسْيَانَ وَمَا اسْتُكْرِهُوا عَلَيْهِ».

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu (madhambi ya) kukosea na kusahau, na yale waliyolazimishwa".

Ibn ‘Abbās (may Allah be pleased with him and his father) reported that the Messenger of Allah (ﷺ) said: "Allah has pardoned for me the mistakes and forgetfulness of my Ummah, and what they were coerced into doing."

Upana wa huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na upole wake kwa waja wake kiasi ambacho amewaondolea madhambi pale yatakapojitokeza maasi katika hali hizi tatu.

Fadhila ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya umma wake.

Kuondolewa dhambi haimaanishi kuondolewa hukumu au dhamana, mfano atakayesahau udhu, na akaswali kwa kudhani kuwa yuko twahara, hana dhambi katika hilo, lakini atatakiwa kutia udhu na kurudia swala.

Lazima katika kuondolewa dhambi kwa kulazimishwa kuwe na sharti, mfano kama akiwa mlazimishaji anauwezo wa kutimiza alichotishia.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih al-Bukhari · Hadith Na. HE-4216 (Aqidah na Misingi ya Imani · Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu)
Daraja na Mpokezi:
Amesema Imamu Nawawi: Hadithi hii ni hasan · Imepokelewa na Ibnu Maajah, Al-Bayhaqi na wengineo
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
bukhari:he:4216