Nyuma

akatawadha mbele yao udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ يحيى بنِ عُمَارةَ المَازِنِيِّ قَالَ: شَهِدْتُ عَمْرَو بْنَ أَبِي حَسَنٍ سَأَلَ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ زَيْدٍ، عَنْ وُضُوءِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَدَعَا بِتَوْرٍ مِنْ مَاءٍ، فَتَوَضَّأَ لَهُمْ وُضُوءَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَكْفَأَ عَلَى يَدِهِ مِنَ التَّوْرِ، فَغَسَلَ يَدَيْهِ ثَلاَثًا، ثُمَّ أَدْخَلَ يَدَهُ فِي التَّوْرِ، فَمَضْمَضَ وَاسْتَنْشَقَ وَاسْتَنْثَرَ، ثَلاَثَ غَرَفَاتٍ، ثُمَّ أَدْخَلَ يَدَهُ فَغَسَلَ وَجْهَهُ ثَلاَثًا، ثُمَّ غَسَلَ يَدَيْهِ مَرَّتَيْنِ إِلَى المِرْفَقَيْنِ، ثُمَّ أَدْخَلَ يَدَهُ فَمَسَحَ رَأْسَهُ، فَأَقْبَلَ بِهِمَا وَأَدْبَرَ مَرَّةً وَاحِدَةً، ثُمَّ غَسَلَ رِجْلَيْهِ إِلَى الكَعْبَيْنِ.

Imepokelewa kutoka kwa Yahya Bin Umaara Al-Maaziniy amesema: Nilimshuhudia Amri Bin Abii Hasan akimuuliza Abdallah Bin Zaidi, kuhusu udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akaagiza bakuli la maji, akatawadha mbele yao udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akamimina katika mikono yake kutoka katika bakuli, akaosha viganja vyake mara tatu, kisha akaingiza mkono wake ndani ya bakuli, akasukutua na akapandisha maji puani na akapenga, kwa michoto mitatu, kisha akaingiza mkono wake akaosha uso wake mara tatu, kisha akaosha mikono yake mara mbili mpaka katika viwiko viwili, kisha akaingiza mkono wake akafuta kichwa chake, akaanza upande wa mbele na akapeleka mpaka nyuma ya kichwa, mara moja, kisha akaosha miguu yake mpaka katika kongo mbili.

Yahya ibn ‘Umārah al-Māzini reported: I witnessed 'Amr ibn Abi Hasan asking 'Abdullah ibn Zayd about the ablution of the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him), so he asked for a vessel of water and performed ablution like that of the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) in front of them. He poured water from the vessel on his hand, washing his hands thrice. Then, he put his hand inside the vessel, rinsed his mouth, sniffed water, and blew it out with three handfuls. He put his hand in the water again and washed his face thrice. Then, he washed his hands twice up to the elbows, after which he put his hand in the water and wiped over his head, bringing them to the front and the back of his head once. Then, he washed his feet up to the ankles.

Tabia za mwalimu ni njia ya karibu zaidi ya kuleta uelewa na kuifanya elimu isisahaulike, na katika hili ni kufundisha kwa vitendo.

Inafaa kurudia mara tatu katika baadhi ya viungo vya udhu na mara mbili katika baadhi yake, na wajibu ni mara moja.

Uwajibu wa kufuata mpangilio kati ya viungo vya udhu kama ilivyokuja katika hadithi.

Kikomo cha uso ni kuanzia maoteo ya nywele, mpaka ndevu za chini na kidevu, kwa urefu, na kuanzia sikio mpaka sikio jingine, kwa upana.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. HE-3444 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:3444