Nyuma

Atakapoota mmoja wenu ndoto anayoipenda basi ndoto hiyo inatoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo, amshukuru Mwenyezi Mungu kwa ndoto hiyo na aisimulie, na akiota ndoto kinyume na hiyo katika yale anayoyachukia, basi ndoto hiyo inatokana na Shetani, basi aombe kinga kutokana na shari yake, na wala asiisimulie kwa yeyote, kwani haitomdhuru

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رضي الله عنه أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «إِذَا رَأَى أَحَدُكُمُ الرُّؤْيَا يُحِبُّهَا فَإِنَّهَا مِنَ اللَّهِ، فَلْيَحْمَدِ اللَّهَ عَلَيْهَا وَلْيُحَدِّثْ بِهَا، وَإِذَا رَأَى غَيْرَ ذَلِكَ مِمَّا يَكْرَهُ، فَإِنَّمَا هِيَ مِنَ الشَّيْطَانِ، فَلْيَسْتَعِذْ مِنْ شَرِّهَا، وَلاَ يَذْكُرْهَا لِأَحَدٍ، فَإِنَّهَا لَنْ تَضُرَّهُ».

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakapoota mmoja wenu ndoto anayoipenda basi ndoto hiyo inatoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo, amshukuru Mwenyezi Mungu kwa ndoto hiyo na aisimulie, na akiota ndoto kinyume na hiyo katika yale anayoyachukia, basi ndoto hiyo inatokana na Shetani, basi aombe kinga kutokana na shari yake, na wala asiisimulie kwa yeyote, kwani haitomdhuru".

Abu Sa‘īd al-Khudri (may Allah be pleased with him) reported that he heard the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) say: "If any of you sees a vision he likes, it is from Allah. So, let him praise Allah for it, and let him recount it. If he sees something else that he dislikes, it is from the devil. So, let him seek refuge from its evil and mention it to no one, for it will not harm him."

Migawanyiko ya ndoto: 1- Ndoto njema, nayo ni ndoto ya kweli na ni habari njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu anayoiona mtu au ikaonwa na mtu mwingine. 2- Mawazo: Nayo ni yale ambayo mtu huwaza mwenyewe akiwa macho. 3- Kutiwa huzuni na hofu na Shetani na vitisho kutoka kwake ili amuhuzunishe mwanadam.

Uhalisia wa haya yaliyotajwa katika mlango wa ndoto njema ni mambo matatu: Amshukuru Mwenyezi Mungu juu ya ndoto hiyo, na ajipe habari njema, na aihadithie, lakini asimueleze ila yule anayempenda nasi anayemchukia.

Na uhalisia wa hayo yaliyotajwa katika adabu za ndoto zenye kuchukiza ni mambo matano: Ajikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake, na kutokana na shari ya Shetani, na ateme kushoto mara tatu pale anaposhituka kutoka usingizini mwake, na wala asiisimulie kamwe kwa yeyote, na anapotaka kurejea katika usingizi wake basi ageukie ubavu mwingine tofauti na ule aliokuwa mwanzo; kwani ndoto hiyo wala haitomdhuru.

Amesema bin Hajari: Hekima na lengo la kukatazwa kumsimulia asiyempenda nikuwa endapo atamsimulia huenda akamfasiria kwa mambo yenye kumchukiza, ima kwa sababu ya chuki au husuda, na huenda ikatokea kwa namna ile ile aliyomfasiria au akajiwahi mwenyewe kwa kuanza kuhuzunika na kukosa furaha, akaamrisha kuacha kumhadithia asiyempenda kwa sababu hiyo.

Kushukuru pale zinapotokea neema, na kujirudiarudia kwa mazuri, hilo ni sababu ya kuyadumisha mazuri hayo.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih al-Bukhari · Hadith Na. 7045 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
bukhari:he:3285