Nyuma

Hakika katika Jihadi kubwa ni kusema neno la uadilifu kwa kiongozi dhalimu

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ مِنْ أَعْظَمِ الجِهَادِ كَلِمَةَ عَدْلٍ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ».

Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika katika Jihadi kubwa ni kusema neno la uadilifu kwa kiongozi dhalimu".

Abu Sa‘īd al-Khudri (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Among the best of Jihad is to speak a word of justice to an oppressive ruler."

Kuamrisha mema na kukataza maovu ni katika Jihadi.

Kumnasihi kiongozi ni katika Jihadi kubwa, lakini ni lazima iwe kwa elimu na hekima na kuwa na uhakika.

Amesema Imam Al-Khattabi: Hii imekuwa jihadi bora kabisa kwa sababu anaye pigana na adui husitasita baina ya kuwa na matumaini na khofu, hajui atashinda au atashindwa, na kiongozi ana mamlaka mkononi mwake, hivyo ikiwa atasema kweli na akamuamrisha mema atakuwa kajitia katika hatari, na kaiweka nafsi yake katika maangamivu, hivyo ikawa ni aina bora ya jihadi kwa sababu ya kushinda khofu, na imesemwa kuwa: Imekuwa ni Jihadi bora; Kwa sababu ikiwa mtawala atachukua neno lake, faida inaweza kuenea kwa idadi kubwa ya watu, na masilahi yatapatikana.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Musnad Ahmad · Hadith Na. HE-3045 (Kulingania Dini na Kujitolea · Kuamrisha Mema na Kukataza Mabaya)
Daraja na Mpokezi:
Ni nzuri kwa sababu ya hadithi nyinginezo · Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
ahmad:he:3045