Nyuma

Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kupi kunusurika? Akasema: "Shika ulimi wako, na ikutoshe nyumba yako, na lia kwa ajili ya makosa yako

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ رضي الله عنه قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ مَا النَّجَاةُ؟ قَالَ: «امْلِكْ عَلَيْكَ لِسَانَكَ، وَلْيَسَعْكَ بَيْتُكَ، وَابْكِ عَلَى خَطِيئَتِكَ».

Kutoka kwa Ukba bin Aamir Al-Juhaniy -radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kupi kunusurika? Akasema: "Shika ulimi wako, na ikutoshe nyumba yako, na lia kwa ajili ya makosa yako".

‘Uqbah ibn ‘Āmir (may Allah be pleased with him) reported: I said: O Messenger of Allah, what is salvation? He said: "Control your tongue, abide in your house, and weep over your sin."

Pupa ya Maswahaba katika kujua njia za kusalimika.

Kumebainishwa sababu za kusalimika katika Dunia na Akhera.

Himizo la mtu kushughulika na nafsi yake anaposhindwa kumnufaisha mtu mwingine, au akahofia madhara juu ya dini yake na nafsi yake endapo atachanganyikana na watu.

Hapa kuna ishara ya kuipa kipaumbele nyumba, na hasa hasa wakati wa fitina, kwani ni katika nyenzo za kuihifadhi dini.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Jami' at-Tirmidhiy · Hadith Na. 2406 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
tirmidhi:hadeethenc:3602