عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ السَّاعِدِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «رِبَاطُ يَوْمٍ فِي سَبِيلِ اللَّهِ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا، وَمَوْضِعُ سَوْطِ أَحَدِكُمْ مِنَ الجَنَّةِ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا، وَالرَّوْحَةُ يَرُوحُهَا العَبْدُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَوِ الغَدْوَةُ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا».
Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad radhi za Allah ziwe juu yake hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Kudumu siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na sehemu ya mjeledi wa mmoja wenu peponi ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na kutoka asubuhi kwa mja katika njia ya Mwenyezi Mungu au kutoka mchana ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake".
Sahl ibn Sa‘d as-Sā‘idi (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Observing Ribāt (guarding the Muslims' frontiers) for one day in the cause of Allah is better than the world and everything in it. The place occupied by the whip of one of you in Paradise is better than the world and everything in it. The evening or morning walk that one takes in the cause of Allah is better than the world and everything in it."
Fadhila za kuthubutu katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu ya hatari zilizomo zinazoihatarisha nafsi, na kwa yale yanayofungamana nalo kama kulinyanyua neno la Mwenyezi Mungu na kuitetea dini yake, kwa hivyo, thawabu za siku moja pekee, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.
Udhalili wa dunia ukiilinganisha na akhera; kwa sababu sehemu ya kuweka mjeledi pekee peponi, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.
Ubora wa kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na ukubwa wa thawabu zake; kwa sababu thawabu za mwendo mmoja wa asubuhi au mchana, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.
Kauli yake: "Katika njia ya Mwenyezi Mungu" hapa kuna dalili ya umuhimu wa kutakasa nia, na kwamba malipo yanaambatana na hilo.