عن أنس بن مالك رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال: "إن عِظَمَ الجزاءِ مع عِظَمِ البلاءِ، وإن الله تعالى إذا أحب قوما ابتلاهم، فمن رَضِيَ فله الرِضا، ومن سَخِطَ فله السُّخْطُ".
Kutoka kwa Anas bin Maliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume rehema na Amani zimfikie, yakuwa yeye Amesema: "Hakika ukubwa wa malipo huendana sawa pamoja na ukubwa wa matatizo, na hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anapowapenda watu huwapa mtihani; atakayeridhia atapata radhi, na atakayechukia atapata hasira (za Mwenyezi Mungu)."
Anas ibn Mālik (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: “The greater the tribulation, the greater the reward. When Allah loves people, He tests them. So whoever is content, for him is pleasure; and whoever is discontent, for him is displeasure.”
Nikuwa matatizo yanafuta madhambi, madam tu hajaambatana na kuacha la wajibu, kama kuacha kuvumilia, au kufanya la haramu kama kuchana nguo na kupiga mashavu.
Kuthibitisha sifa ya mapenzi kwa Mwenyezi Mungu kwa namna inayoendana na Utukufu wake.
Hakika matatizo kwa Muumini ni katika alama za Imani.
Kuthibitisha sifa ya kuridhia na kuchukia kwa Mwenyezi Mungu kwa namna inayoendana na Utukufu wake.
Kupendeza kuridhika na hukumu ya Mwenyezi Mungu na makadirio yake.
kuharamishwa kukasirikia hukumu ya Mwenyezi Mungu na makadirio yake.
Kuhimizwa kuvumilia juu ya matatizo.
Mwanadamu anaweza kuchukia jambo nalo likawa na kheri.
Kuthibitisha hekima kwa Mwenyezi Mungu katika vitendo vyake.
Malipo huendana na matendo.