عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما: أَنَّ نَبِيَّ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَقُولُ عِنْدَ الْكَرْبِ: «لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ الْعَظِيمُ الْحَلِيمُ، لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ، لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَرَبُّ الْأَرْضِ وَرَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ».
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema wakati wa matatizo: "Laa ilaaha illa llaahul a'dhwiimul haliim, Laa ilaaha illa llaahu Rabbul A'rshil A'dhwiim, Laa ilaaha illa llaahu Rabbu ssamaawaati warabbul A'rshil kariim" Tafsiri: Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mpole, Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola wa A'rshi tukufu, Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola wa mbingu, na Mola wa ardhi, na Mola wa A'rshi takatifu".
Ibn ‘Abbās (may Allah be pleased with him and his father) reported: The Prophet of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) used to say during times of distress: "There is no god but Allah, the Most Great, the Forbearing. There is no god but Allah, the Lord of the Mighty Throne. There is no god but Allah, the Lord of the heavens, the Lord of the earth, and the Lord of the Noble Throne."
Uwajibu wa kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu kwa dua wakati wa kufikwa na misiba na matatizo.
Kupendeza kuomba dua hii wakati wa matatizo.
Arshi ya Rahmaan (Mwingi wa rehema) aliyotulizana juu yake Aliyetakasika na kutukuka, ndio kiumbe cha juu zaidi kuliko vyote, na kikubwa zaidi na kitukufu zaidi kuliko vyote, na alitoa wasifu wake Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ni kubwa na ni tukufu.
Zimetajwa mbingu na ardhi pekee; kwa sababu ni katika viumbe vikubwa zaidi katika vile vinavyoonekana.
Amesema Attwayyibi: Ametanguliza sifa hii kwa kumtaja Mola Mlezi ili iendane na kutatua shida; kwa sababu ndilo neno linaloendana na malezi, na ndani yake kuna tahlil (kauli ya Laa ilaaha illa llaah) iliyokusanya tauhidi ambayo ndiyo asili ya kutakasa utukufu wake, na utukufu ambao unaonyesha utimilifu wa uwezo, na upole ambao unaonyesha kuwa na elimu, kwa sababu mjinga hatuwezi kuvuta picha kuwa anaweza kuwa na upole wala ukarimu kwa vitu asivyovijua, nazo ndio asili ya sifa na ukarimu.