عَنْ أَبِي رُقَيَّةَ تَمِيمِ بْنِ أَوْسٍ الدَّارِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «الدِّينُ النَّصِيحَةُ» قُلْنَا: لِمَنْ؟ قَالَ: «لِلهِ وَلِكِتَابِهِ وَلِرَسُولِهِ وَلِأَئِمَّةِ الْمُسْلِمِينَ وَعَامَّتِهِمْ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ruqaiyya Tamim Ausi Ad-dari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Dini ni nasaha" Tukasema: Kwa ajili ya nani? Akasema: "Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kitabu chake, na Mtume wake, na kwa viongozi wa waislamu na watu wote."
Abu Ruqayyah Tamīm ibn Aws ad-Dāri (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (ﷺ) said: "Religion is sincerity." We said: "To whom?" He said: "To Allah, to His Book, to His Messenger, to the Muslim leaders and their common folk."
Amri ya kunasihiana ni kwa watu wote.
Ukubwa na utukufu wa nafasi ya nasaha katika dini.
Dini imekusanya mambo ya itikadi, maneno, na matendo.
Miongoni mwa nasaha ni kujinasihi mwenyewe kutomfanyia udanganyifu yule mwenye kunasihiwa pamoja na kumtakia kheri.
Uzuri wa mafundisho ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kiasi kwamba anataja jambo kwa ujumla kisha analifafanua.
Kuanza na lenye umuhimu zaidi kisha linalofuata, kwani alianza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa nasaha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha kitabu chake, kisha Mtume wake -Rehema na amani ziwe juu yake- kisha viongozi wa waislamu, kisha watu wote kwa ujumla.