عَنْ أُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: كَانَ رَجُلٌ لَا أَعْلَمُ رَجُلًا أَبْعَدَ مِنَ الْمَسْجِدِ مِنْهُ، وَكَانَ لَا تُخْطِئُهُ صَلَاةٌ، قَالَ: فَقِيلَ لَهُ: أَوْ قُلْتُ لَهُ: لَوْ اشْتَرَيْتَ حِمَارًا تَرْكَبُهُ فِي الظَّلْمَاءِ، وَفِي الرَّمْضَاءِ، قَالَ: مَا يَسُرُّنِي أَنَّ مَنْزِلِي إِلَى جَنْبِ الْمَسْجِدِ، إِنِّي أُرِيدُ أَنْ يُكْتَبَ لِي مَمْشَايَ إِلَى الْمَسْجِدِ، وَرُجُوعِي إِذَا رَجَعْتُ إِلَى أَهْلِي، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «قَدْ جَمَعَ اللهُ لَكَ ذَلِكَ كُلَّهُ».
Kutoka kwa Ubai bin Ka'ab radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Kulikuwa na mtu ambaye sifahamu kama kuna mtu alikuwa akiishi mbali kuliko yeye, na swala ilikuwa haimpiti, akaambiwa: Bora ungelinunua Punda ukimpanda nyakati za giza, na unapopita kwenye sehemu ya jangwa. Akasema: "Hainifurahishi nyumba yangu kuwa karibu na Msikiti, mimi ninapenda niandikiwe malipo ya kutembea kwangu, na kurudi kwangu ninaporejea kwa Watu wangu" Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu amekukusanyia malipo yote hayo".
’Ubayy ibn Ka‘b (may Allah be pleased with him) reported: There was a man who, as far as I know, lived farther from the mosque than anyone else, and he never missed a prayer. He said: It was said to him, or I said to him: If only you would buy a donkey so that you may ride it in the darkness and the scorching heat. He said: I do not like that my house be near the mosque, for I want the steps I take to the mosque and back from it to my family to be recorded for me. Upon this, the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Verily, Allah has gathered all of that for you."
Pupa kubwa ya Maswahaba juu ya kheri na kuzidisha zaidi na kuchuma malipo.
Amesema Nawawi: Hapa kumethibitishwa thawabu katika hatua wakati wa kurudi kutoka katika swala kama zinavyopatikana katika kwenda.
Kuelezana waislamu mambo ya heri na kuusiana wema, atakayeona ndugu yake kuwa anapatwa na tabu basi amfuate na amnasihi kuziondoa tabu hizo.
Nyumba kuwa mbali na msikiti si udhuru wa kuacha swala ya jamaa, maadamu mtu anasikia Adhana.