Nyuma

Jambo la kwanza alilioanza kupewa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake katika wahyi, ni njozi nzuri (za kweli) usingizini

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنِينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْها أَنَّهَا قَالَتْ: أَوَّلُ مَا بُدِئَ بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنَ الوَحْيِ الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ فِي النَّوْمِ، فَكَانَ لاَ يَرَى رُؤْيَا إِلَّا جَاءَتْ مِثْلَ فَلَقِ الصُّبْحِ، ثُمَّ حُبِّبَ إِلَيْهِ الخَلاَءُ، وَكَانَ يَخْلُو بِغَارِ حِرَاءٍ فَيَتَحَنَّثُ فِيهِ -وَهُوَ التَّعَبُّدُ- اللَّيَالِيَ ذَوَاتِ العَدَدِ قَبْلَ أَنْ يَنْزِعَ إِلَى أَهْلِهِ، وَيَتَزَوَّدُ لِذَلِكَ، ثُمَّ يَرْجِعُ إِلَى خَدِيجَةَ فَيَتَزَوَّدُ لِمِثْلِهَا، حَتَّى جَاءَهُ الحَقُّ وَهُوَ فِي غَارِ حِرَاءٍ، فَجَاءَهُ المَلَكُ فَقَالَ: اقْرَأْ، قَالَ: «مَا أَنَا بِقَارِئٍ» قَالَ: «فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الجَهْدَ ثُمَّ أَرْسَلَنِي، فَقَالَ: اقْرَأْ، قُلْتُ: مَا أَنَا بِقَارِئٍ، فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّانِيَةَ حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الجَهْدَ ثُمَّ أَرْسَلَنِي، فَقَالَ: اقْرَأْ، فَقُلْتُ: مَا أَنَا بِقَارِئٍ، فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّالِثَةَ ثُمَّ أَرْسَلَنِي، فَقَالَ: {اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ خَلَقَ الإِنْسَانَ مِنْ عَلَقٍ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الأَكْرَمُ}»، [العلق:1-3] فَرَجَعَ بِهَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَرْجُفُ فُؤَادُهُ، فَدَخَلَ عَلَى خَدِيجَةَ بِنْتِ خُوَيْلِدٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، فَقَالَ: «زَمِّلُونِي، زَمِّلُونِي» فَزَمَّلُوهُ حَتَّى ذَهَبَ عَنْهُ الرَّوْعُ، فَقَالَ لِخَدِيجَةَ وَأَخْبَرَهَا الخَبَرَ: «لَقَدْ خَشِيتُ عَلَى نَفْسِي» فَقَالَتْ خَدِيجَةُ: كَلَّا وَاللَّهِ مَا يُخْزِيكَ اللَّهُ أَبَدًا، إِنَّكَ لَتَصِلُ الرَّحِمَ، وَتَحْمِلُ الكَلَّ، وَتَكْسِبُ المَعْدُومَ، وَتَقْرِي الضَّيْفَ، وَتُعِينُ عَلَى نَوَائِبِ الحَقِّ، فَانْطَلَقَتْ بِهِ خَدِيجَةُ حَتَّى أَتَتْ بِهِ وَرَقَةَ بْنَ نَوْفَلِ بْنِ أَسَدِ بْنِ عَبْدِ العُزَّى، ابْنَ عَمِّ خَدِيجَةَ، وَكَانَ امْرَأً تَنَصَّرَ فِي الجَاهِلِيَّةِ، وَكَانَ يَكْتُبُ الكِتَابَ العِبْرَانِيَّ، فَيَكْتُبُ مِنَ الإِنْجِيلِ بِالعِبْرَانِيَّةِ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكْتُبَ، وَكَانَ شَيْخًا كَبِيرًا قَدْ عَمِيَ، فَقَالَتْ لَهُ خَدِيجَةُ: يَا ابْنَ عَمِّ، اسْمَعْ مِنَ ابْنِ أَخِيكَ، فَقَالَ لَهُ وَرَقَةُ: يَا ابْنَ أَخِي، مَاذَا تَرَى؟ فَأَخْبَرَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَبَرَ مَا رَأَى، فَقَالَ لَهُ وَرَقَةُ: هَذَا النَّامُوسُ الَّذِي نَزَّلَ اللَّهُ عَلَى مُوسَى، يَا لَيْتَنِي فِيهَا جَذَعًا، لَيْتَنِي أَكُونُ حَيًّا إِذْ يُخْرِجُكَ قَوْمُكَ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَوَ مُخْرِجِيَّ هُمْ؟»، قَالَ: نَعَمْ، لَمْ يَأْتِ رَجُلٌ قَطُّ بِمِثْلِ مَا جِئْتَ بِهِ إِلَّا عُودِيَ، وَإِنْ يُدْرِكْنِي يَوْمُكَ أَنْصُرْكَ نَصْرًا مُؤَزَّرًا. ثُمَّ لَمْ يَنْشَبْ وَرَقَةُ أَنْ تُوُفِّيَ، وَفَتَرَ الوَحْيُ.

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Jambo la kwanza alilioanza kupewa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake katika wahyi, ni njozi nzuri (za kweli) usingizini. Akawa haoti njozi isipokuwa itatokea, mfano wa mapambazuko ya asubuhi, kisha akapendezeshwa kujitenga peke yake katika pango la Hira, akawa akitawa huko - ambako ni kuabudu - kwa siku kadhaa, kabla ya kurejea katika familia yake, na alikuwa akichukua chakula cha kutosha kwa ajili ya hilo, kisha alikuwa akirudi kwa Khadija na kumpatia chakula mfano wa hicho, mpaka ukweli ukamjia akiwa ndani ya pango la Hira, Malaika akamjia, akasema: "Soma!" akasema: “Mimi si msomaji.” Akanichukua na akanifunika mpaka nikachoka, kisha akaniacha, akasema: "Soma!" Nikasema: “Mimi sio msomaji". Basi akanichukua na akanifunika mara ya pili mpaka nikapatwa na uchovu, kisha akaniacha, kisha akasema: "Soma!" nikasema: "Mimi si msomaji", basi akanichukua na akanifunika kwa mara ya tatu, kisha akaniacha, na akasema: "Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba Amemuumba mwanadamu kwa pande la damu Soma na Mola wako Mlezi ni Mkarimu" [Al-Alaq: 1-3] Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akarudi huku moyo wake ukitetemeka, akaingia kwa Khadija binti Khuwailidi, Allah amuwiye radhi, na akasema: “Nisaidieni, kuwa pamoja nami, Nisaidieni, kuwa pamoja nami” Basi wakamkumbatia mpaka hofu ikamtoka, basi akamwambia Khadija na kumueleza habari hiyo: “Nilihofia sana nafsi yangu" Khadija akasema: Hapana, Wallahi kamwe Mwenyezi Mungu hatokufedhehesha, hakika wewe utaunga udugu, utamsaidia mnyonge, na utaleta kilichokosekana, na utamkirimu mgeni, na utasaidia wakati wa matatizo ya haki, basi Khadija akaondoka naye mpaka wakafika kwa Waraqa bin Nawfal bin Asad bin Abdil-Uzza, binamu yake Khadija, na alikuwa ni mtu aliyeingia katika Ukristo wakati wa kabla ya Uislamu, na alikuwa akiandika vitabu vya Kiebrania, hivyo aliandika kutoka katika Injili kwa Kiebrania, kiasi alichotaka Mwenyezi Mungu akiandike, alikuwa mzee ambaye amekwisha pofuka, basi Khadija akamwambia: Ewe binamu, sikia kutoka kwa mtoto wa ndugu yako. Waraqa akamuuliza: Ewe mpwa wangu, unaona nini? Basi Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akamueleza aliyoyaona. Waraqa akamwambia: Hii ndiyo sheria aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu kwa Musa. Hakika ninatamani ningekuwa hai wakati watu wako, pindi watakapokufukuza watu wako. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Hivi, kwani watanifukuza!?" Akasema: "Ndiyo" Kamwe hakuwahi kuja mtu na kitu kama ulichokuja nacho, isipokuwa alitendewa uadui, na ikiwa siku yako hiyo itanifikia nikiwa hai, basi nitakutetea utetezi wa nguvu. Kisha Waraqa hakuchukua muda mrefu akawa amefariki, na wahyi ukasimama kuteremka kwa muda.

‘Ā’ishah, Mother of the Believers, (may Allah be pleased with her) reported: The first thing the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) started to experience from the revelation was the good vision in his sleep. He never saw a vision except that it came true like the break of dawn. Then seclusion was endeared to him, and he used to retreat to the Cave of Hirā’, where he would engage in Tahannuth-which is worship—for several nights before returning to his family and taking provisions for this. He would then go back to Khadījah to take provisions again for a similar number of nights until the truth came to him while he was in the Cave of Hirā’. The Angel came to him and said: Read! He said: "I do not know how to read." He said: "He took hold of me and pressed me forcefully until I could no longer bear it and then released me, saying: Read! I said: I do not know how to read. He took hold of me and pressed me forcefully for the second time until I could no longer bear it and then released me, saying: Read! I said: I do not know how to read. He took hold of me and pressed me forcefully for the third time and then released me, saying: {Read in the name of your Lord Who created, created man from a clinging clot. Read, and your Lord is the Most Generous.}" [Surat al-‘Alaq: 1-3] The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) returned with these while his heart was trembling. He entered upon Khadījah bint Khuwaylid (may Allah be pleased with her) and said: "Cover me! Cover me!" They covered him until the shock of fear was gone from him. Then he informed Khadījah of what had happened and said to her: "Indeed, I feared for myself." Khadījah said: No, by Allah, Allah will never fail you. Verily, you maintain kinship ties, help those in need, support the destitute, provide the guests with food and shelter, and assist those affected by calamities. Khadījah took him to her cousin Waraqah ibn Nawfal ibn Asad ibn ‘Abdul-‘Uzza, who had embraced Christianity in the pre-Islamic period and used to write the Scripture in Hebrew. He would write from the Gospel in Hebrew as much as Allah wished him to write. He was an old man and had lost his eyesight. Khadījah said to him: O my cousin, listen to what your nephew has to say. Waraqah said to him: O my nephew, what have you seen? The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) informed him of what he had seen. Waraqah said to him: This is the same Nāmūs (i.e., the angel) whom Allah had sent to Moses. I wish I were young and could live until the time when your people would drive you out. The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Would they drive me out?" Waraqah said: Yes. No one has ever come with something like what you have brought without being treated with hostility. If I should live until that day, I would support you strongly. Soon after, Waraqah passed away, and the revelation paused.

Hapa kumebainishwa mwanzo wa wahyi kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Njozi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni miongoni mwa aina za wahyi.

Sheria ya kuchukua akiba ya mahitaji, na kwamba hilo haliendi kinyume na kumtegemea Mwenyezi Mungu, kwani alilifanya hilo mbora wa wenye kumtegemea Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake.

Ukamilifu wa ukarimu wake Aliyetakasika na kutukuka, kwa sababu aliwafundisha waja wake wasiyoyajua, na akawahamisha kutoka katika giza la ujinga kwenda katika nuru ya elimu.

Fadhila za kujua kuandika; kwa sababu ndani yake kuna manufaa makubwa yasiyohesabika; kwani kwa hilo elimu zimaendikwa, na hukumu zikawekewa mipaka, na habari za wa mwanzo zikadhibitiwa, na vikahifadhiwa vitabu vya Mwenyezi Mungu vilivyoteremshwa, na yakanyooka mambo ya dini na dunia.

Maneno ya mwanzo kuteremka katika Qur'ani ni "Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliyeumba" [Al-Alaq: 1].

Tabia njema na mambo ya kheri ni sababu ya kusalimika na majanga mabaya, na aina mbalimbali za kero, zitakayekithiri kheri zake basi utakuwa mzuri mwisho wake, na unatarajiwa kwake usalama wa dini na dunia.

Hapa inaonyesha kuwa; inafaa kumsifia mtu mbele yake kukiwa na masilahi.

Ni wajibu kumliwaza aliyepatwa na mambo ya kuogofya, na kumpa habari njema, na kumueleza sababu za kusalimika na hilo.

Ushahidi mkubwa na uthibitisho ulio wazi kabisa wa ukamilifu wa Khadija, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, na ukubwa wa rai yake, na nguvu ya nafsi yake, na ukubwa wa elimu yake ya kisheria, ni kwamba katika maelezo yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikusanya kila aina ya msingi wa wema, na muhimili wake, kwa sababu wema ima uwe kwa ndugu wa karibu, au kwa watu baki, au uwe kwa mwili, au kwa fedha, au kwa mwenye jukumu, au uwe kwa mtu mwingine, na alipanua mazungumzo yake katika hilo kwa ni mahali panapofaa kufanya hivyo, kwa ajili ya mlolongo wa maneno mengine.

Mtu yeyote atakayefikwa na jambo, inapendeza amueleze mtu anayemuamini katika nasaha zake na rai yake.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih al-Bukhari · Hadith Na. 3 (Historia na Wasifu wa Mtume ﷺ · Maisha ya Mtume na Maswahaba)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
bukhari:he:66303