Nyuma

Msimlaani, Wallahi, namuapa Mwenyezi Mungu sikujua lolote kwake isipokuwa anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ عُمَرَ بْنِ الخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: أَنَّ رَجُلًا عَلَى عَهْدِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ اسْمُهُ عَبْدَ اللَّهِ، وَكَانَ يُلَقَّبُ حِمَارًا، وَكَانَ يُضْحِكُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَكَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَدْ جَلَدَهُ فِي الشَّرَابِ، فَأُتِيَ بِهِ يَوْمًا فَأَمَرَ بِهِ فَجُلِدَ، فَقَالَ رَجُلٌ مِنَ القَوْمِ: اللَّهُمَّ الْعَنْهُ، مَا أَكْثَرَ مَا يُؤْتَى بِهِ؟ فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لاَ تَلْعَنُوهُ، فَوَاللَّهِ مَا عَلِمْتُ أَنَّهُ يُحِبُّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ».

Imepokelewa kutoka kwa Omari bin Khattwab -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kwamba mtu mmoja alikuwa katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake jina lake anaitwa Abdallah, na alikuwa akitaniwa kwa jina la Punda, na alikuwa akimchekesha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekwisha mchapa viboko kwa sababu ya ulevi, basi akaletwa siku moja akaamrisha akachapwa, akasema mtu mmoja katika jamaa waliopo: Ewe Mwenyezi Mungu mlaani, ni mara ngapi analetwa!? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Msimlaani, Wallahi, namuapa Mwenyezi Mungu sikujua lolote kwake isipokuwa anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake".

‘Umar ibn al-Khattāb (may Allah be pleased with him) reported: A man at the time of the Prophet (ﷺ), whose name was ‘Abdullah and who was nicknamed Himār, used to make the Messenger of Allah (ﷺ) laugh. The Prophet (ﷺ) had flogged him for drinking (intoxicants). One day, he was brought again, and the Prophet (ﷺ) ordered that he be flogged. Then a man from among the people said: O Allah, curse him! How often is he brought? The Prophet (ﷺ) said: "Do not curse him, for by Allah, I know that he loves Allah and His Messenger."

Haipingani kati ya kufanya makatazo na kuthibiti kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndani ya moyo wa mwenye kuyafanya; kwa sababu yeye rehema na amani ziwe juu yake ameeleza kuwa huyo aliyetajwa katika hadithi anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake pamoja na hayo yaliyojitokeza kwake.

Mtenda madhambi makubwa atakapokufa na huku anaendelea na chochote katika hayo huyo atakuwa chini ya matashi, akitaka Mwenyezi Mungu atamsamehe na akitaka atamuadhibu, na habakishwi milele motoni yeyote katika Waislamu.

Inachukiza kumlaani mnywa pombe; kwa kutaraji kuwa huenda kukawa na kizuizi cha kutompata laana; kwa sababu kumlaani mtu maalumu na kumuombea dua mbaya, huenda hilo likampelekea katika ujeuri, au likamkatisha tamaa ya kukubaliwa toba.

Inafaa kulaani bila kumuanisha mtu kwa hilo.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih al-Bukhari · Hadith Na. 6780 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
bukhari:he:66214