Nyuma

Walikuja watu kutoka kabila la Ukli au Uraina, wakauchukia mjini Madina

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَدِمَ أُنَاسٌ مِنْ عُكْلٍ أَوْ عُرَيْنَةَ، فَاجْتَوَوْا المَدِينَةَ فَأَمَرَهُمُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِلِقَاحٍ، وَأَنْ يَشْرَبُوا مِنْ أَبْوَالِهَا وَأَلْبَانِهَا، فَانْطَلَقُوا، فَلَمَّا صَحُّوا قَتَلُوا رَاعِيَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَاسْتَاقُوا النَّعَمَ، فَجَاءَ الخَبَرُ فِي أَوَّلِ النَّهَارِ، فَبَعَثَ فِي آثَارِهِمْ، فَلَمَّا ارْتَفَعَ النَّهَارُ جِيءَ بِهِمْ، فَأَمَرَ فَقَطَعَ أَيْدِيَهُمْ وَأَرْجُلَهُمْ، وَسُمِرَتْ أَعْيُنُهُمْ، وَأُلْقُوا فِي الحَرَّةِ، يَسْتَسْقُونَ فَلاَ يُسْقَوْنَ، قَالَ أَبُو قِلاَبَةَ: فَهَؤُلاَءِ سَرَقُوا وَقَتَلُوا، وَكَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ، وَحَارَبُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ.

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Walikuja watu kutoka kabila la Ukli au Uraina, wakauchukia mjini Madina, kwa sababu hali ya hewa ya Madina haikuwafaa. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaamuru waende katika ngamia wa zaka na wanywe mikojo yake na maziwa yake. Wakaondoka, na baada ya afya yao kurejea, wakamuua mchungaji wa ngamia wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wakaiba ngamia hao. Habari zikamfikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake mapema asubuhi, basi akatuma watu kuwafuatilia, na wakapatikana kabla ya mchana. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaamuru mikono na miguu yao ikatwe, macho yao yakachomwa moto, na wakatupwa kwenye jangwa la mawe (Al-Harra). Wakawa wakiomba maji, lakini hawakupewa. Abu Qilaba anasema: Watu hawa walifanya wizi, wakafanya mauaji, walitoka katika Uislamu baada ya kuwa Waislamu, na walitangaza vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.

Anas ibn Mālik (may Allah be pleased with him) reported: Some people from ‘Ukl or ‘Uraynah came, and the climate of Madīnah did not suit them, so they became ill. The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) ordered them with the milch camels and drink from their urine and milk. They left, and when they recovered, they killed the herdsman of the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) and drove off the camels. The news came early in the day, so he sent people in pursuit of them. When the sun had risen, they were brought back. He ordered that their hands and feet be cut off and their eyes be branded, and they were thrown into Al-Harrah, where they begged for water but were not given any. Abu Qilābah said: They stole, killed, disbelieved after embracing faith, and waged war against Allah and his Messenger.

Usafi wa mkojo wa kila kinacholiwa nyama yake.

Sheria ya kujitibu kwa maziwa ya ngamia na mikojo yake.

Sheria ya kufananisha katika kisasi, na katazo la kusulubu litachukuliwa pale panapokuwa hakuna mfanano na kisasi.

Kuua kundi la watu kwa sababu ya mtu mmoja ni sawa, iwe walimuuwa kwa hila au kwa wizi wa kutumia silaha.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih al-Bukhari · Hadith Na. 233 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
bukhari:he:66205