عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «تَابِعُوا بَيْنَ الحَجِّ وَالعُمْرَةِ، فَإِنَّهُمَا يَنْفِيَانِ الفَقْرَ وَالذُّنُوبَ كَمَا يَنْفِي الكِيرُ خَبَثَ الحَدِيدِ، وَالذَّهَبِ، وَالفِضَّةِ، وَلَيْسَ لِلْحَجَّةِ الْمَبْرُورَةِ ثَوَابٌ إِلاَّ الجَنَّةُ».
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Fuatanisheni kati ya Hija na Umra, kwani huondoa umasikini na madhambi kama moto unavyoondoa uchafu wa chuma, na dhahabu, na fedha, na haina Hija nzuri na safi malipo isipokuwa Pepo".
‘Abdullah ibn Mas‘ūd (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Perform Hajj and ‘Umrah in succession, for they expel poverty and sins just as the bellows expels impurities from iron, gold, and silver. There is no reward for an accepted Hajj except Paradise."
Fadhila za kufuatanisha baina ya Hija na umra na himizo katika hilo.
Kufuatanisha kati ya Hija na Umra ni miongoni mwa sababu za utajiri na msamaha wa madhambi.
Amesema Al-Mubaarakafuriy: (Huondoa umasikini) Yaani: Huuondosha kabisa, na hii inategemea maana zote mbili: Umasikini unaoonekana kwa kupatikana utajiri wa mkononi, na umasikini wa ndani, kwa kupata utajiri wa moyo.