Nyuma

Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa anapo swali anatanua kati ya mikono yake mpaka unaonekana weupe wa kwapa zake

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَالِكٍ ابْنِ بُحَيْنَةَ رضي الله عنه: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ إِذَا صَلَّى فَرَّجَ بَيْنَ يَدَيْهِ حَتَّى يَبْدُوَ بَيَاضُ إِبْطَيْهِ.

Kutoka kwa Abdallah bin Maliki bin Buhaina radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa anapo swali anatanua kati ya mikono yake mpaka unaonekana weupe wa kwapa zake.

Abdullah ibn Mālik ibn Buhaynah (may Allah be pleased with him) reported: When the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) prayed, he used to spread out his hands until the whiteness of his armpits would be visible.

Mkao huu unapendeza katika sijida, nao ni kuweka mbali vikwapa na mbavu.

Maamuma ambaye jirani yake anakereka kwa kutanua kwake mikono; si sheria kwake kufanya hivyo.

Katika kutanua mikono katika sijida, kuna hekima na faida nyingi, miongoni mwake ni: kuonyesha uchangamfu na hamu ya kusali, na kwamba ikiwa mtu ataegemea viungo vyote katika sijida, kila kiungo kitapata sehemu yake ya ibada. Ikasemwa kuwa: Hekima katika hili ni kuwa ni sawa na unyenyekevu, na inafaa zaidi katika kuweka paji la uso na pua karibu na ardhi, na pia ili kila kiungo kiweze kutofautishwa peke yake.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. HE-3220 (Muslim — bado haijapangwa (ya muda) · Hadith zilizogunduliwa hivi karibuni (ya muda))
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili (jina la mtafsiri halijatajwa katika API) · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:hadeethenc-provisional:3220