Nyuma

Mwenye kuisoma Qur'ani kwa sauti ya wazi ni kama mwenye kutoa sadaka hadharani, na mwenye kuisoma Qur'ani kwa siri ni kama mwenye kuficha sadaka

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عن عُقبة بن عامر الجُهني رضي الله عنه قال: قال رسولُ الله صلَّى الله عليه وسلم: «الجاهِرُ بالقرآن كالجاهِرِ بالصَّدَقَةِ، والمُسِرُّ بالقرآن كالمُسِرِّ بالصَّدَقَة».

Imepokelewa kutoka kwa Uqbah Bin Aamir Al-juhaniy-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake: "Mwenye kuisoma Qur'ani kwa sauti ya wazi ni kama mwenye kutoa sadaka hadharani, na mwenye kuisoma Qur'ani kwa siri ni kama mwenye kuficha sadaka."

‘Uqbah ibn ‘Āmir al-Juhani (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah’s peace and blessings be upon him) said: "He who recites the Qur’an openly is like he who gives charity openly, and he who recites the Qur’an secretly is like he who gives charity secretly."

Kuficha usomaji wa Qur'ani ni bora, kama ilivyo kuficha sadaka ni bora zaidi, kwa kuwa kufanya hivyo ni katika utakasifu wa nia na kujiweka mbali na kujionesha na kujisikia, isipokuwa itakapohitajika, na maslahi ya kuisoma kwa wazi ni katika kuifundisha.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sunan an-Nasa'i · Hadith Na. HE-65055 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
nasai:he:65055