Nyuma

Atakayesema wakati anasikia adhana: Allaahumma rabba haadhihid da'watit taamma, was swalaatul qaaima, aati Muhammadanil wasiilata wal fadhwiila, wab'ath-huu maqaaman mahmuudanil ladhii wa a'ttah, (Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wa wito huu uliotimia, na swala iliyosimama, mpe Muhammad utetezi na fadhila, na umfufue mahali pakusifiwa ulipomuahidi) basi utakuwa halali kwake utetezi wangu siku ya Kiyama

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رضي الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ قَالَ حِينَ يَسْمَعُ النِّدَاءَ: اللَّهُمَّ رَبَّ هَذِهِ الدَّعْوَةِ التَّامَّةِ، وَالصَّلاَةِ القَائِمَةِ، آتِ مُحَمَّدًا الوَسِيلَةَ وَالفَضِيلَةَ، وَابْعَثْهُ مَقَامًا مَحْمُودًا الَّذِي وَعَدْتَهُ، حَلَّتْ لَهُ شَفَاعَتِي يَوْمَ القِيَامَةِ».

Na kutoka kwa Jaabir bin Abdillah -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayesema wakati anasikia adhana: Allaahumma rabba haadhihid da'watit taamma, was swalaatul qaaima, aati Muhammadanil wasiilata wal fadhwiila, wab'ath-huu maqaaman mahmuudanil ladhii wa a'ttah, (Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wa wito huu uliotimia, na swala iliyosimama, mpe Muhammad utetezi na fadhila, na umfufue mahali pakusifiwa ulipomuahidi) basi utakuwa halali kwake utetezi wangu siku ya Kiyama".

Jābir ibn ‘Abdullah (may Allah be pleased with him and his father) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Whoever says upon hearing the call: O Allah, Lord of this perfect call and the prayer that is to be established, grant Muhammad Al-Wasīlah and Al-Fadīlah and resurrect him to the Praiseworthy Station that You have promised him, he will be granted my intercession on the Day of Judgment."

Sheria ya kuomba dua hii baada ya kumaliza kurudia nyuma ya muadhini, na ambaye hatosikia adhana; basi hatakiwi kuisema.

Ubora wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kiasi kwamba amepewa uwakala na fadhila na nafasi na utetezi mkuu wa kutetea kuhukumiwa baina ya viumbe.

Kuthibitisha utetezi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake; kwa kauli yake: "Ataupata utetezi wangu siku ya Kiyama".

Utetezi wake rehema na amani ziwe juu yake utakuwa kwa wale waliotenda madhambi makubwa katika umma wake ili wasiingie motoni, au aliyeingia atoke, au katika kuingia peponi pasina hesabu, au kunyanyuliwa daraja aliyeingia.

Amesema Attwayyibi: kuanzia mwanzo wa "Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu" huu ndio wito uliotimia, na maneno "Hayya a'la" (njooni katika) ndio swala iliyosimama katika kauli yake wanasimamisha swala, na inawezekana kuwa makusudio ya swala hapa ni dua, na kwa mujibu wa hili kauli yake "na swala iliyosimama" ni kubainishwa wito uliyotimia, na inawezekana kuwa makusudio yake ni swala iliyozoeleka wanayoitwa kwayo kwa wakati huo, na ndilo lililokaribu na maana halisi.

Amesema Al-Mulhab: Katika hadithi hii kuna himizo la kuomba dua katika nyakati za swala; kwa sababu ni hali zinazotarajiwa zaidi kujibiwa dua.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih al-Bukhari · Hadith Na. 614 (Aqidah na Misingi ya Imani · Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
bukhari:he:10635