Nyuma

Atakapoamka mmoja wenu kutoka usingizini mwake basi na apenge kwa maji mara tatu, kwani Shetani hulala ndani ya tundu zake za pua

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا اسْتَيْقَظَ أَحَدُكُمْ مِنْ مَنَامِهِ فَلْيَسْتَنْثِرْ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، فَإِنَّ الشَّيْطَانَ يَبِيتُ عَلَى خَيَاشِيمِهِ».

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapoamka mmoja wenu kutoka usingizini mwake basi na apenge kwa maji mara tatu, kwani Shetani hulala ndani ya tundu zake za pua".

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "If any of you wakes up from his sleep, let him blow water out of his nose three times, as the devil spends the night on his nostrils."

Anaweka sheria kwa kila mwenye kuamka kutoka usingizini apenge ili kuondoa athari za Shetani puani mwake, na endapo kama atatawadha, hapo amri ya kupenga itakuwa ni lazima.

Kupenga ni katika faida kamili ya kupandisha maji puani; na kupenga kunatoa uchafu huo kupitia maji.

Kufungamanisha na usingizi wa usiku pekee, kwa kuchukua kutoka katika tamko "Kulala" kwani kulala huwa hakuwi ila kwa usingizi wa usiku, kwa sababu ndio usingizi wa kulala muda mrefu na wa fofofo.

Katika hadithi kuna dalili kuwa Shetani humgusa mwanadam pasina yeye kulihisi hilo.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 238 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:8377