Nyuma

Fanyeni haraka kufanya matendo kuna fitina nzito kama kipande cha usiku wa giza,

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «بَادِرُوا بِالْأَعْمَالِ فِتَنًا كَقِطَعِ اللَّيْلِ الْمُظْلِمِ، يُصْبِحُ الرَّجُلُ مُؤْمِنًا وَيُمْسِي كَافِرًا، أَوْ يُمْسِي مُؤْمِنًا وَيُصْبِحُ كَافِرًا، يَبِيعُ دِينَهُ بِعَرَضٍ مِنَ الدُّنْيَا».

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Fanyeni haraka kufanya matendo kuna fitina nzito kama kipande cha usiku wa giza, anaamka mtu akiwa muislamu anafika jioni akiwa kafiri, na anashinda akiwa muumini anaamka asubuhi akiwa kafiri, anauza dini yake kwa thamani ndogo ya dunia"

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Hasten to deeds before being overtaken by tribulations that are like patches of the darkest night; a man would be a believer in the morning and become a disbeliever in the evening, or he would be a believer in the evening and become a disbeliever in the morning. He sells his religion for a worldly gain."

Ni lazima kushikamana na dini, na kwenda mbio katika matendo mema kabla ya vikwazo kuzuia hilo.

Hii ni ishara ya mfuatano wa majaribu yenye kupoteza katika zama za mwisho, na kwamba wakati wowote fitina moja inapotoweka, fitina ingine linafuata.

Ikiwa dini ya mtu ni dhaifu na akaiacha kwa kubadilishana na mambo ya kidunia, kama vile pesa au vitu vingine, hii ni sababu ya kupotoka kwake, kuacha dini, na kuingia kwake kwenye vishawishi na fitina.

Kuna ushahidi katika Hadithi kwamba matendo mema ni njia ya kuokoka na fitina.

Kuna aina mbili za fitina: Fitina ya shubuha (Mambo yenye utata), na tiba yake ni elimu, na fitina ya matamanio, na tiba yake ni imani na subira.

Hadithi inaashiria kuwa mwenye matendo kidogo, fitina kwake ni nyepesi zaidi, na mwenye matendo mengi anatakiwa asihadaike na alichonacho, bali aongeze zaidi.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 118 (Muslim — bado haijapangwa (ya muda) · Hadith zilizogunduliwa hivi karibuni (ya muda))
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa Imamu Muslim
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili (jina la mtafsiri halijatajwa katika API) · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:hadeethenc-provisional:3138