عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ اللَّهَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى يَقُولُ لِأَهْلِ الجَنَّةِ: يَا أَهْلَ الجَنَّةِ؟ فَيَقُولُونَ: لَبَّيْكَ رَبَّنَا وَسَعْدَيْكَ، فَيَقُولُ: هَلْ رَضِيتُمْ؟ فَيَقُولُونَ: وَمَا لَنَا لاَ نَرْضَى وَقَدْ أَعْطَيْتَنَا مَا لَمْ تُعْطِ أَحَدًا مِنْ خَلْقِكَ؟ فَيَقُولُ: أَنَا أُعْطِيكُمْ أَفْضَلَ مِنْ ذَلِكَ، قَالُوا: يَا رَبِّ، وَأَيُّ شَيْءٍ أَفْضَلُ مِنْ ذَلِكَ؟ فَيَقُولُ: أُحِلُّ عَلَيْكُمْ رِضْوَانِي، فَلاَ أَسْخَطُ عَلَيْكُمْ بَعْدَهُ أَبَدًا».
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: “Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na Kutukuka, atawaambia watu wa Peponi: Enyi watu wa Peponi? Watasema: Labeka tumekuitikia na umetukuka, atasema: Je, mmeridhika? Watasema: Tuna nini mpaka tusiridhike hali yakuwa umetupa mambo ambayo hujampa yeyote katika viumbe wako? Atasema: Mimi nitakupeni kilicho bora zaidi kuliko hilo, Watasema: Ewe Mola Mlezi, ni kitu gani kilicho bora kuliko hili? Atasema: Ninawapeni radhi zangu, wala sitowachukia baada yake milele".
Abu Sa‘īd al-Khudri (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Allah Almighty will say to the dwellers of Paradise: 'O people of Paradise!' They will reply: 'O our Lord, we present ourselves and are at Your pleasure.' He will say: ‘Are you contented?’ They will say: 'How could we not be contented, O Lord, when You have given us what You have not given to any of Your creation?' He will say: 'I shall give you something better than that?’ They will say: 'O Lord, what could be better than that?' He will say: 'I shall bestow My pleasure upon you and I shall not be displeased with you ever after that.'"
Mazungumzo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu pamoja na watu wa peponi.
Habari njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa watu wa peponi ya kuwaridhia, na kuwateremshia radhi juu yao na kutochukia tena milele.
Kila mtu Peponi ataridhika na hali yake licha ya kutofautiana viwango vyao na kupishana daraja zao; Kwa sababu wote walijibu kwa neno moja, ambalo ni: "Umetupa kile ambacho hukumpa yeyote katika viumbe vyako."