عَنْ سَلْمَانَ الْفَارِسِيِّ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «ثَلَاثَةٌ لَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ: أُشَيْمِطٌ زَانٍ، وَعَائِلٌ مُسْتَكْبِرٌ، وَرَجُلٌ جَعَلَ اللَّهَ لَهُ بِضَاعَةً، فَلَا يَبِيعُ إِلَّا بِيَمِينِهِ وَلَا يَشْتَرِي إِلَّا بِيَمِينِهِ».
Na kutoka kwa Salmani Alfaaris -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Watu wa aina tatu hatowasemesha Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama wala hatowatakasa na watakuwa na adhabu chungu, Mzee mzinifu, na masikini jeuri, na mtu aliyemfanya Mwenyezi Mungu kuwa ndio bidhaa, hauzi ila kwa kiapo chake wala hanunui ila kwa kiapo chake".
Salmān al-Fārisi (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "There are three to whom Allah will not speak on the Day of Judgment, nor will He purify them, and they will incur a painful punishment: an aged person who commits adultery, a poor person who is arrogant, and a man whom Allah has given a commodity, yet he does not sell except by swearing an oath, nor buy except by swearing an oath."
Amesema Kadhi Iyadhi katika sababu ya adhabu hii kali: Nikuwa kila mmoja miongoni mwao alishikamana na maasi haya yaliyotajwa pamoja nakuwa yuko mbali nayo, na hapakuwa na haja ya kufanya hivyo, na udhaifu wa vishawishi vyake kwake; hata kama hakuna anayepewa udhuru wa kufanya dhambi, lakini kwa sababu hapakuwa na haja ya kutenda maasi haya yenye kukera, wala kishawishi kilichozoeleka, hii inafanana na ukaidi, na kudharau haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akaamua kumuasi si kwamba ana haja ya kufanya hivyo.
Zinaa na uongo na kiburi ni katika madhambi makubwa.
Kiburi: Ni kukataa haki, na kuwadharau viumbe.
Tahadhari ya kukithirisha kutumia kiapo katika kuuza na kununua, na himizo la kuheshimu kiapo, na kuheshimu majina ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, amesema Mtukufu: "Na wala msifanye Mwenyezi Mungu katika viapo vyenu kuwa kisingizio cha kuacha kufanya wema" [Baqara: 224].