Nyuma

Kiapo hutoa bidhaa, na hufuta faida

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَن أَبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «الْحَلِفُ مَنْفَقَةٌ لِلسِّلْعَةِ، مَمْحَقَةٌ لِلرِّبْحِ».

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Kiapo hutoa bidhaa, na hufuta faida".

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: I heard the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) say: "An oath is a means for selling a commodity and a means for destroying the profit."

Ukubwa wa swala la kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, na kwamba hakuwi ila kwa haja.

Kipato cha haramu hata kama kitakuwa kingi; basi hicho kimeondolewa baraka wala hakina kheri ndani yake.

Amesema Qaari: Kuondoka kwa baraka za kipato; ima kwa uharibifu unaoweza kutokea katika mali yake, au kwa kuitoa katika mambo ambayo hanufaiki nayo katika dunia au thawabu Akhera, au zikabakia kwake lakini akanyimwa kunufaika nazo, au akazirithi ambaye hatomshukuru.

Amesema Nawawi: Hapa kuna katazo la kukithirisha kuapa katika biashara, kwa sababu kuapa pasina haja ni machukizo, na linaambatana hilo na kupambia bidhaa, na huenda mnunuzi akadanganyika na kiapo.

Kukithirisha viapo ni upungufu wa imani, na ni upungufu wa tauhidi; kwa sababu kukithirisha viapo kuna pelekea mambo mawili: La kwanza: Kupuuza hilo na kutojali, la pili: Uongo, kwa sababu mwenye kukithiri viapo vyake huingia katika uongo, ni lazima kupunguza na kutokithirisha viapo, na ndio maana alisema Mtukufu: "Na hifadhini viapo vyenu" [Maaida: 89].

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih al-Bukhari · Hadith Na. 2087 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
bukhari:he:5936