Nyuma

Nikuwa Talbiya (kuitika) kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kulikuwa ni: Labbaikallaahumma labbaika -Nimekuitikia ewe Mola nimekutikia, Labbaika laa shariika laka labbaika -Nimekuitikia huna mshirika wako nimekuitikia, Hakika sifa njema na neema zote ni zako pamoja na ufalme, wewe pekee usiye na mshirika

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا: أَنَّ تَلْبِيَةَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَبَّيْكَ اللهُمَّ، لَبَّيْكَ، لَبَّيْكَ لَا شَرِيكَ لَكَ لَبَّيْكَ، إِنَّ الْحَمْدَ وَالنِّعْمَةَ لَكَ وَالْمُلْكَ لَا شَرِيكَ لَكَ» قَالَ: وَكَانَ عَبْدُ اللهِ بْنُ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا يَزِيدُ فِيهَا: لَبَّيْكَ لَبَّيْكَ، وَسَعْدَيْكَ، وَالْخَيْرُ بِيَدَيْكَ، لَبَّيْكَ وَالرَّغْبَاءُ إِلَيْكَ وَالْعَمَلُ.

Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-: "Nikuwa Talbiya (kuitika) kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kulikuwa ni: Labbaikallaahumma labbaika -Nimekuitikia ewe Mola nimekutikia, Labbaika laa shariika laka labbaika -Nimekuitikia huna mshirika wako nimekuitikia, Hakika sifa njema na neema zote ni zako pamoja na ufalme, wewe pekee usiye na mshirika.". Amesema: Na alikuwa Abdallah bin Omari akizidisha ndani yake: "Labbaika Labbaika wasa'daika, -Nimekuitikia nimekuitikia na utukufu ni wako, wal khairu biyadaika, -Na heri iko mikono mwako, na hamu zote na matendo mwisho ni kwako".

‘Abdullah ibn ‘Umar (may Allah be pleased with him and his father) reported: The Talbiyah of the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him): "Labbayka Allāhumma labbayk, labbayka la sharīka laka labbayk, inna al-hamda wa an-ni‘mata laka wal-mulk, la sharīka lak." (O Allah, I respond to Your call, I do respond. I respond to Your call, You have no partner, I do respond. Verily, praise, blessing, and sovereignty belong to You; You have no partner) He said: ‘Abdullah ibn ‘Umar (may Allah be pleased with him and his father) used to add: Labbayka labbayka, wa sa‘dayka, wa al-khayru biyadayk. Labbayka wa ar-raghbā’u ilayka wa al-‘amal (I respond to Your call, I respond to Your call, and I ask You to make me happy.) Goodness is in Your Hands. I respond to Your call, and to You belong desires and actions).

Sheria ya kuleta talbiya (muitikio) katika Hija na Umra, na mkazo wake ndani yake; kwa sababu hiyo ndiyo nembo yake maalumu, kama ambavyo takbiri (Allaahu Akbar) ni nembo ya swala.

Amesema bin Munir: Na katika sheria ya talbiya kuna ukumbusho juu ya ukarimu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake kuwa misafara yao kwenda katika Al-kaaba ilikuwa ni kwa wito maalum kutoka kwake Aliyetakasika na kutukuka.

Kilicho bora ni kushikamana na talbiya ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hakuna tatizo kuongeza, kwa kukiri kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika hilo, amesema bin Hajari: Na hii ndio namna ya uadilifu zaidi, kwa kusema pekee maneno yalikuja kwa kuchukuliwa moja kwa moja kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akichagua kauli iliyokuja kutoka kwa swahaba pekee, au akaanzisha mwenyewe katika yale yanayofaa, yeye mwenyewe peke yake ili maneno yasichanganyike na yale yaliyonukuliwa kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hii inafanana na hali ya dua katika tahiyatu, kwani alisema katika dua hiyo: Kisha achague katika maombi na sifa azitakazo: Yaani baada ya kumaliza ile iliyofundishwa.

Sunna ya kunyanyua sauti katika talbiya, na hii ni kwa wanaume, ama mwanamke atashusha sauti yake kwa kuhofia fitina.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 1184 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:4535