Maktaba

MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

🌙 Mwezi wa Qur'ani na Rehema

Ramadhan Al-Mubarak

Mwongozo wa mafundisho sahihi ya Mtume Muhammad ﷺ, dua za mfungo na fadhila za mwezi mtukufu.

Kuelekea Ramadhan 1448 AH Takriban 8 Februari 2027
-- Siku
:
-- Masaa
:
-- Dakika
:
-- Sekunde

Mwandamo rasmi wa mwezi hutangazwa kulingana na kuonekana kwa hilali ya mwezi mtukufu.

Dua za Kila Siku za Mfungo

Dua ya Kufungua Swawm (Kufuturu)
ذَهَبَ الظَّمَأُ، وَابْتَلَّتِ الْعُرُوقُ، وَثَبَتَ الأَجْرُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ
"Dhahaba adh-dhama'u, wabtallat al-'urooqu, wa thabata al-ajru in sha' Allaah."
"Kiu kimeondoka, na mishipa imelowa, na ujira umethibiti akipenda Mwenyezi Mungu."
Abu Dawud Na. 2357 · Sahih
Dua ya Kufuturishwa na Mtu / Ugeni
أَفْطَرَ عِنْدَكُمُ الصَّائِمُونَ، وَأَكَلَ طَعَامَكُمُ الأَبْرَارُ، وَصَلَّتْ عَلَيْكُمُ الْمَلاَئِكَةُ
"Aftara 'indakumu as-saa'imoona, wa akala ta'aamakumu al-abraaru, wa sallat 'alaykumu al-malaa'ikah."
"Wafungue kwenu waliofunga, na wale chakula chenu wacha-Mungu, na wawaombee rehema Malaika."
Abu Dawud Na. 3854 · Sahih
Dua ya Laylatul Qadr (Masiku 10 ya Mwisho)
اللَّهُمَّ إِنَّكَ عَفُوٌّ تُحِبُّ الْعَفْوَ فَاعْفُ عَنِّي
"Allaahumma innaka 'Afuwwun tuhibbu al-'afwa fa'fu 'anniy."
"Ewe Mwenyezi Mungu, hakika Wewe ni Mwenye kusamehe, Unapenda msamaha, basi nisamehe mimi."
At-Tirmidhi Na. 3513 · Sahih

Hadithi Sahihi za Ramadhani

Milango ya Pepo Kufunguliwa
إِذَا دَخَلَ شَهْرُ رَمَضَانَ فُتِّحَتْ أَبْوَابُ السَّمَاءِ، وَغُلِّقَتْ أَبْوَابُ جَهَنَّمَ، وَسُلْسِلَتِ الشَّيَاطِينُ

Amesema Mtume Muhammad ﷺ: "Unapoingia mwezi wa Ramadhani, hufunguliwa milango ya Mbingu (Pepo), na hufungwa milango ya Moto (Jahannam), na hufungwa minyororo Mashetani."

Sahih al-Bukhari Na. 1899 · Sahih Muslim Na. 1079
Msamaha wa Dhambi Zilizotangulia
مَنْ صَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ

Amesema Mtume Muhammad ﷺ: "Atakayefunga Ramadhani kwa Imani na kutarajia malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, atasamehewa dhambi zake zilizotangulia."

Sahih al-Bukhari Na. 38 · Sahih Muslim Na. 760