Pindi nilipopandishwa juu mbinguni, nilipita kwa watu wakiwa na kucha za shaba, wakizikwarua kwazo nyuso zao na vifua vyao
Wema, Uadilifu na Tabia Njema
Kiarabu
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَمَّا عُرِجَ بِي مَرَرْتُ بِقَوْمٍ لَهُمْ أَظْفَارٌ مِنْ نُحَاسٍ يَخْمُشُونَ بها وُجُوهَهُمْ وَصُدُورَهُمْ، فَقُلْتُ: مَنْ هَؤُلَاءِ يَا جِبْرِيلُ، قَالَ: هَؤُلَاءِ الَّذِينَ يَأْكُلُونَ لُحُومَ النَّاسِ، وَيَقَعُونَ فِي أَعْرَاضِهِمْ».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Pindi nilipopandishwa juu mbinguni, nilipita kwa watu wakiwa na kucha za shaba, wakizikwarua kwazo nyuso zao na vifua vyao, nikasema: Ni akina nani hao ewe Jibrili, akasema: Hawa ni wale wanaokula nyama za watu, na wanajitumbukiza katika kuvunja heshima za watu".
English translation
Anas ibn Mālik (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "When I was taken on an ascent to heaven, I passed by a group of people (in Hellfire) with copper nails scratching their faces and chests. I asked: O Gabriel, who are these? He replied: These are the ones who eat the flesh of people (by backbiting) and slander them."
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ya kwamba yeye pindi alipopandishwa juu mbinguni usiku Israa na Miiraji (safari ya usiku na kupandishwa), alipita kwa watu wakiwa na kucha za shaba wakizikwarua na kuzichana kwazo nyuso zao na vifua vyao, akamuuliza rehema na amani ziwe juu yake Jibril amani iwe juu yake: Ni kitu gani walifanya hawa mpaka wanalipwa kwa adhabu hii? Akasema Jibril amani iwe juu yake: Hawa ni wale wanaosengenya watu, na wanazungumza vibaya kuhusu heshima zao pasina haki.
Faida
- Tahadhari kubwa ya kusengenya, na amefananishwa msengenyaji na mtu anayekula nyama ya mtu.
- Kutia dosari heshima za watu ni katika kuwasengenya na mfano wake ni katika madhambi makubwa.
- Amesema Attwayibi: Katika kauli yake: "Wakizikwarua", Amesema: Kwa sababu kukwarua uso na kifua ni miongoni mwa sifa za wanawake wanaoomboleza kwa mayowe, basi Mwenyezi Mungu akazifanya kuwa ndio malipo ya mwenye kusengenya na kuchafua heshima za Waislamu, akionyesha kuwa hizo si katika sifa za wanaume, bali hizo ni katika sifa za wanawake wakiwa katika hali mbaya zaidi na sura mbaya mno.
- Uwajibu wa kuamini ghaibu na yale yote aliyoyaeleza Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.