Yeyote atakayetoka katika kutafuta elimu basi huyo yuko katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka atakaporejea.
Wema, Uadilifu na Tabia Njema
Kiarabu
عن أنس رضي الله عنه مرفوعاً: «من خَرج في طلب العلم فهو في سَبِيلِ الله حتى يرجع».
Tafsiri ya Kiswahili
Kutoka kwa Anas Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake hadithi Marfu'u: "Yeyote atakayetoka katika kutafuta elimu basi huyo yuko katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka atakaporejea".
English translation
Anas (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: “Whoever goes out to seek knowledge is in the cause of Allah until he returns.”
Maelezo
Maana ya hadithi: Nikuwa atakayetoka nyumbani kwake au katika mji wake; kwaajili ya kutafuta elimu ya kisheria,huyo anakuwa katika hukumu ya aliyetoka kwaajili ya Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu,mpaka atakaporudi kwa watu wake; kwasababu anakuwa ni kama mpiganaji katika kuihuisha kwake dini na kumdhalilisha shetani na kuitaabisha nafsi.
Faida
- Nikuwa kutafuta elimu ni kupambana katika njia ya Mwenyezi Mungu.
- Mwenye kutafuta elimu ana malipo ya mpiganaji katika viwanja vya mapambano; kwasababu wote hao wanayasimamia yale yanayoweza kuipa nguvu sheria ya Mwenyezi Mungu na wanazuia yasiyokuwa humo.
- Ndani yake nikuwa mwenye kutoka katika kutafuta elimu atakuwa na malipo ya kutembea kwake na kwenda kwake na kurudi kwake mpaka atakaporejea kwa watu wake.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.