Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Jami' at-Tirmidhiy · Na. HE-3587

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Assalaam alaikum, akamjibu, kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kumi

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: السَّلَامُ عَلَيْكُمْ، فَرَدَّ عَلَيْهِ ثُمَّ جَلَسَ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «عَشْرٌ» ثُمَّ جَاءَ آخَرُ فَقَالَ: السَّلَامُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللَّهِ، فَرَدَّ عَلَيْهِ فَجَلَسَ، فَقَالَ: «عِشْرُونَ» ثُمَّ جَاءَ آخَرُ فَقَالَ: السَّلَامُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ، فَرَدَّ عَلَيْهِ فَجَلَسَ، فَقَالَ: «ثَلَاثُونَ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Imran bin Huswaini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Assalaam alaikum, akamjibu, kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kumi" Kisha akaja mwingine akasema: Assalaam alaikum warahmatullaah, akamjibu, akakaa, akasema: "Ishirini" Kisha akaja mtu mwingine akasema: Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh, akamjibu akakaa, akasema: "Thelathini".

English translation

‘Imrān ibn Husayn (may Allah be pleased with him) reported: A man came to the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) and said: As-salāmu ‘alaykum (peace be upon you). He responded to him and then sat down. The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Ten." Then another came and said: As-salāmu ‘alaykum wa rahmatullāh (may the peace and mercy of Allah be upon you). He responded to him and so he sat down. He said: "Twenty." Then another came and said: As-salāmu ‘alaykum wa rahmatullāh wa barakātuh (may the peace, mercy, and blessings of Allah be upon you). He responded to him and so he sat down. He said: "Thirty."

Maelezo

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Assalaam alaikum" Akamjibu kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ameandikiwa mema kumi, kisha akaja mtu mwingine akasema: "Assalaam alaikum warahmatullaahi" Akamjibu, kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Amepata thawabu ishirini, kisha akaja mwingine akasema: "Assalaam alaikum warahmatullahi wabarakaatuh", akamjibu akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kapata thawabu thelathini; yaani kwa kila tamko ni mema kumi.

Faida

  • Anayefika awaanze waliokaa kwa salamu.
  • Malipo kuongezeka kwa kuzidi matamshi ya salamu.
  • Ukamilifu katika kutoa salamu: "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh", na namna nzuri katika kujibu: Ni "Waalaikumus salaam warahmatullaahi wabarakaatuh".
  • Daraja za kutoa salamu na kujibu zinatofautiana, vile vile malipo yanatofautiana.
  • Kuwafundisha watu kheri na kuwatanabahisha ili kufanya lililobora zaidi.
  • Amesema bin Hajari: Ikiwa atazidisha mwenye kuanza "Warahmatullah" basi ni sunna kwake "wabarakaatuh", na ikiwa atazidisha "wabarakaatuh" je ni sheria pia kuzidisha wakati wa kujibu? Na vile vile ikiwa atazidisha mwenye kuanza "wabarakaatuh" je ni sheria kwake kufanya hivyo, ameitoa Maliki katika Muwattwa'a kutoka kwa bin Abbasi radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Salamu imeishia katika baraka.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)