Atakapokutana mmoja wenu na ndugu yake basi na amsalimie, ukiwatenganisha kati yao mti, au ukuta, au jiwe, kisha akakutana naye tena basi amsalimie tena
Wema, Uadilifu na Tabia Njema
Kiarabu
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا لَقِيَ أَحَدُكُمْ أَخَاهُ فَلْيُسَلِّمْ عَلَيْهِ، فَإِنْ حَالَتْ بَيْنَهُمَا شَجَرَةٌ أَوْ جِدَارٌ أَوْ حَجَرٌ ثُمَّ لَقِيَهُ فَلْيُسَلِّمْ عَلَيْهِ أَيْضًا».
Tafsiri ya Kiswahili
Kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapokutana mmoja wenu na ndugu yake basi na amsalimie, ukiwatenganisha kati yao mti, au ukuta, au jiwe, kisha akakutana naye tena basi amsalimie tena"
English translation
Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "When any of you meets his brother, let him greet him with peace. If a tree, a wall, or a rock comes between them and then he meets him, let him greet him with peace again."
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake anamhimiza muislamu kumsalimia ndugu yake muislamu kila anapokutana naye, hata kama wakiwa wanatembea pamoja na kikawatenganisha chochote, kama mti au ukuta au jiwe kubwa, kisha akakutana naye baada ya hapo basi amsalimie kwa mara nyingine.
Faida
- Ni sunna kusambaza salam, na irudiwerudiwe kila hali inapobadilika.
- Pupa yake kubwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kusambaza sunna ya salam na kukithirisha; kwakuwa ndani yake kuna kuleta mapenzi na kuzoeana kati ya waislamu.
- Salaam ni kusema: "Assalaam alaikum" Amani iwe nanyi, au "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh", Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi na rehema zake na baraka zake", hii ni tofauti na kupeana mkono kunakotokea mara ya kwanza wakati wa kukutana.
- Salam ni dua, na waislamu wanahaja kubwa ya kuombeana wao kwa wao hata kama litajirudiarudia hilo.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.