Atakapofika mmoja wenu katika kikao basi na atoe salamu, na akitaka kunyanyuka pia atoe salamu, kwani ya mwanzo haina haki zaidi kuliko ya mwisho
Wema, Uadilifu na Tabia Njema
Kiarabu
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِذَا انْتَهَى أَحَدُكُمْ إِلَى الْمَجْلِسِ فَلْيُسَلِّمْ، فَإِذَا أَرَادَ أَنْ يَقُومَ فَلْيُسَلِّمْ، فَلَيْسَتِ الْأُولَى بِأَحَقَّ مِنَ الْآخِرَةِ».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapofika mmoja wenu katika kikao basi na atoe salamu, na akitaka kunyanyuka pia atoe salamu, kwani ya mwanzo haina haki zaidi kuliko ya mwisho".
English translation
Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "When one of you arrives at a gathering, let him greet with peace. When he wants to leave, let him greet with peace, for the first is not more deserving than the last."
Maelezo
Alimuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekuja mahali walipokaa watu basi awasalimie, na akitaka kunyanyuka basi awaage jamaa zake pia kwa salamu; kwani salamu ya kwanza wakati wa kuja si bora sana kuliko salamu ya mwisho wakati wa kuondoka.
Faida
- Himizo la kusambaza salamu.
- Himizo la kuwasalimia jamaa waliokaa wakati wa kukutana nao na wakati wa kuondoka.
- Amesema Assanadi: Kauli yake: "Na akitaka kunyanyuka" Yaani: Kutoka katika kikao, "Salamu Ya mwanzo haina haki zaidi" Yaani: Zote mbili ni sunna halisi zinazotakiwa kufanyiwa kazi, hakuna hiyari ya kuiacha ya pili na kuthibitisha ya kwanza.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.