Muslim — bado haijapangwa (ya muda)
SOMO · Sahih Muslim · Na. 1708

Hapigwi mtu zaidi ya viboko kumi isipokuwa kama itakuwa katika kutelekeza sheria miongoni mwa sharia za Mwenyezi Mungu

Hadith zilizogunduliwa hivi karibuni (ya muda)

Kiarabu

عَنْ أَبِي بُرْدَةَ الْأَنْصَارِيِّ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «لَا يُجْلَدُ أَحَدٌ فَوْقَ عَشَرَةِ أَسْوَاطٍ إِلَّا فِي حَدٍّ مِنْ حُدُودِ اللهِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hapigwi mtu zaidi ya viboko kumi isipokuwa kama itakuwa katika kutelekeza sheria miongoni mwa sharia za Mwenyezi Mungu".

English translation

Abu Burdah al-Ansāri (may Allah be pleased with him) reported that he heard the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) say: "No one should be flogged more than ten lashes except when it comes to one of the limits set by Allah."

Maelezo

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kupigwa mtu yeyote zaidi ya viboko kumi isipokuwa katika maasi, na pia hakuna maelekezo yoyote yaliyokuja katika sheria kueleza idadi maalumu ya viboko au kipigo au adhabu maalumu, na makusudio yake haizidishwi katika kipigo cha kuadabisha zaidi ya viboko kumi, kama kumpiga mke au mtoto.

Faida

  • Mipaka ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyoiamrisha au aliyoikataza inaadhabu zinazokomesha hayo, ima zimepangwa katika sheria, au zinarudi kukadiriwa kwake katika masilahi anayoyaona hakimu.
  • Kutia adabu kunakuwa kwa kiasi kidogo, kwa kiasi cha kuelekeza na kuhofisha, kusizidishwe zaidi ya viboko kumi ikibidi kufanya hivyo, na kilichobora zaidi ni kuwaadabisha pasina kuwapiga, bali kwa kuwaelekeza, na kuwafundisha, na kuwaongoza, na kuwatia hamasa, hilo huleta msukumo mkubwa wa kukubali na upole katika kujifunza, na hali katika nafasi hii hutofautiana sana, inapasa mtu afanye kinachofaa.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)