Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Jami' at-Tirmidhiy · Na. 3464

Atakayesema: Sub-haanallaahi wabihamdi, (Ametakasika Mwenyezi Mungu Mtukufu na sifa njema ni zake) ataoteshewa mti wa mtende peponi

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ جَابِرٍ رَضيَ اللهُ عنهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ قَالَ: سُبْحَانَ اللهِ العَظِيمِ وَبِحَمْدِهِ، غُرِسَتْ لَهُ نَخْلَةٌ فِي الجَنَّةِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayesema: Sub-haanallaahi wabihamdi, (Ametakasika Mwenyezi Mungu Mtukufu na sifa njema ni zake) ataoteshewa mti wa mtende peponi".

English translation

Jābir (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Whoever says: Subhānallāh al-‘azhīm wa bihamdih (Glory be to Allah the Most Great and praise is due to Him), a date palm will be planted for him in Paradise."

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa atakayesema: "Ametakasika Mwenyezi Mungu" ninamtakasa "Mtukufu" kwa dhati yake na sifa zake na vitendo vyake "na sifa njema ni zake" zikiwa zimeambatanishwa na kuegemeza sifa za ukamilifu wake Mtukufu; atasimikiwa na kupandiwa mti wa mtende katika ardhi ya Pepo kwa kila mara atakayosema.

Faida

  • Himizo la kukithirisha kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, na miongoni mwake: Ni kufanya tasbihi na tahmidi (kumtukuza na kumsifu).
  • Pepo ni pana, na kwamba mimea yake ni tasbihi na tahmidi (Kumtuza na kumsifu), na hii ni fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na neema yake.
  • Umetajwa mtende pekee katika hadithi pasina miti mingine; kwa sababu ya wingi wa faida zake na uzuri wa matunda yake; na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu amepiga mfano wa muumini na imani yake ndani ya Qur'ani kwa mti huo.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)