Bukhari — bado haijapangwa (ya muda)
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 3463

Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa kabla yenu, akakasirishwa nalo akachukua kisu akaukata mkono wake, damu ikachuruzika na wala haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, na mimi nimemharamishia pepo

Hadith zilizogunduliwa hivi karibuni (ya muda)

Kiarabu

عَن الحَسَنِ قال: حَدَّثنا جُنْدَبُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ رضي الله عنه، فِي هَذَا المَسْجِدِ، وَمَا نَسِينَا مُنْذُ حَدَّثَنَا، وَمَا نَخْشَى أَنْ يَكُونَ جُنْدُبٌ كَذَبَ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلّى الله عليه وسلم: «كَانَ فِيمَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ رَجُلٌ بِهِ جُرْحٌ، فَجَزِعَ، فَأَخَذَ سِكِّينًا فَحَزَّ بِهَا يَدَهُ، فَمَا رَقَأَ الدَّمُ حَتَّى مَاتَ، قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: بَادَرَنِي عَبْدِي بِنَفْسِهِ، حَرَّمْتُ عَلَيْهِ الجَنَّةَ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Hassan amesema: Alituhadithi Jundab bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake, ndani ya Msikiti huu, na hatujasahahu tangu alivyotuhadithia, na wala hatuhofii kuwa Jundab alimsemea uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alisema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa kabla yenu, akakasirishwa nalo akachukua kisu akaukata mkono wake, damu ikachuruzika na wala haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, na mimi nimemharamishia pepo".

English translation

Al-Hasan reported: Jundab ibn ‘Abdullah (may Allah be pleased with him) narrated to us in this mosque, and we have not forgotten since he narrated to us, nor do we fear that Jundub would have lied about the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him). He said: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Among those who were before you, there was a man who had an injury. He was impatient, so he took a knife and made a cut in his hand and bled to death. Allah Almighty said: My slave hastened to bring about his demise; I have forbidden Paradise for him."

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kulikuwa na mtu katika wale waliokuwa kabla yetu alipatwa na jeraha, akakasirishwa nalo na wala hakuvumilia maumivu, akachukua kisu akaukata mkono wake na akakiharakisha kifo, damu haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, basi nimemharamishia kwake pepo.

Faida

  • Fadhila za kuvumilia balaa, na kuacha kuchukia na kulalamikia maumivu, ili hilo lisipelekee katika jambo baya zaidi kuliko hilo.
  • Kuhadithia kuhusu Umma zilizopita kwa yale ambayo yana kheri na mawaidha ndani yake.
  • Amesema bin Hajari: Hapa kuna kusimama katika haki za Mwenyezi Mungu na rehema zake na kwa viumbe wake, kiasi ambacho amewaharamishia kujiua, na kwamba nafsi ni milki ya Mwenyezi Mungu.
  • Uharamu wa kutumia sababu zinazopelekea katika kuia nafsi, na onyo kali katika hilo.
  • Amesema bin Hajari: Na imeonyesha kuwa alijikata kwa ajili ya kujiua na si kwa kutaka kujitibu, ambayo inaweza kuwa dhana ya kunufaika na kitendo hicho.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)