Imani
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 10

Muislamu wa kweli ni yule wanayepata Amani waislamu wenzake kutokana na ulimi wake na mkono wake, na mhamaji ni yule mwenye kuyahama yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu

Hadithi ya 4: Imani

Kiarabu

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «المُسْلِمُ مَنْ سَلِمَ المُسْلِمُونَ مِنْ لِسَانِهِ وَيَدِهِ، وَالمُهَاجِرُ مَنْ هَجَرَ مَا نَهَى اللَّهُ عَنْهُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Abdillah Bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Muislamu wa kweli ni yule wanayepata Amani waislamu wenzake kutokana na ulimi wake na mkono wake, na mhamaji ni yule mwenye kuyahama yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu".

English translation

‘Abdullah ibn ‘Amr (may Allah be pleased with him and his father) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "A Muslim is the one from whose tongue and hand Muslims are safe, and a Muhājir (emigrant) is the one who abandons what Allah has forbidden."

Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa muislamu mwenye Uislamu kamili ni yule waliosalimika waislamu kutokana na ulimi wake, hawatukani, na wala hawalaani, wala hawasengenyi, na wala hawazunguki kwa aina yoyote miongoni mwa aina za maudhi kwa ulimi wake, na wamesalimika kutokana na mkono wake, hawatendei ubaya, na wala hachukui mali zao pasina haki, na mfano wa hayo, na mwenye kuhama, ni yule mwenye kuacha yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Faida

  • Ukamilifu wa Uislamu hauwi isipokuwa kwa kutofanyia maudhi watu wengine, kwa vitendo au kwa hila yoyote.
  • Ametaja ulimi na mkono pekee pasina viungo vingine; kwa sababu ya wingi wa makosa yake na madhara yake, kwani shari nyingi hutokea kupitia viwili hivi.
  • Himizo la kuacha maasi na kushikamana na yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Muislamu bora kuliko wote ni yule mwenye kutekeleza haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na haki za waislamu.
  • Uadui unaweza kuwa kwa kauli au kitendo.
  • Kuhama kuliko kamilika ni kuyahama aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)