Kwani hawaharamishi aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayaharamisha? na wanahalalisha aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayahalalisha? Nikasema: Ndivyo, Akasema: Basi huko ndiko kuwaabudu.
Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu
Kiarabu
عن عدي بن حاتم رضي الله عنه : "أنه سمع النبي صلى الله عليه وسلم يقرأ هذه الآية: "اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِنْ دُونِ اللَّهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُوا إِلاَّ لِيَعْبُدُوا إِلَهًا وَاحِدًا لا إِلَهَ إِلاَّ هُوَ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ" فقلت له: إنا لسنا نعبدهم، قال: أليس يُحَرِّمُونَ ما أحل الله فتُحَرِّمُونَهُ؟ ويُحِلُّونَ ما حَرَّمَ الله فتُحِلُّونَهُ؟ فقلت: بلى، قال: فتلك عبادتهم".
Tafsiri ya Kiswahili
Kutoka kwa Adiy bin Hatim-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alimsikia Mtume rehema na Amani ziwe juu yake Akisoma aya hii: "Wamewafanya wanachuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu kinyume na Mwenyezi Mungu na Masihi mwana wa Mariam, na hawakuamrishwa ila ni kumuabudu Mungu mmoja, hapana Mola ispokuwa yeye, ametakasika na yale wanayomshirikisha nayo" Nikasema kumwambia: Hakika sisi hatuwaabudu wao, Akasema: "Kwani hawaharamishi aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayaharamisha? na wanahalalisha aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayahalalisha? Nikasema: Ndivyo, Akasema: Basi huko ndiko kuwaabudu".
English translation
‘Adiyy ibn Hātim (may Allah be pleased with him) reported: I heard the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) recite this verse: {They have taken their scholars and monks as lords besides Allah, and [also] the Messiah, the son of Mariyam. And they were not commanded except to worship one God; there is no deity except Him. Exalted is He above whatever they associate with Him.} So I said to him: "We do not worship them." He replied: "Don't they forbid what Allah allows, so you forbid it? Don't they allow what Allah forbids, so you allow it?" I said: 'Yes.' He said: "That is how you worship them."
Maelezo
Aliposikia swahaba huyu mtukufu kisomo cha Mtume rehema na Amani zimfikie cha Aya hii ambayo ndani yake kuna habari kwa Mayahudi na wakristo: kuwa wao wamewafanya wanachuoni wao na wachamungu wao kuwa miungu, wanawawekea sheria zinazokwenda kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu na wakawatii juu ya hilo, ikamtatiza maana yake, kwasababu yeye alikuwa akidhania kuwa ibada inaishia katika kusujudu na mfano wake, Mtume rehema na Amani zimfikie akambainishia- kuwa katika kuwaabudu wanachuoni na watawa: ni kuwatii katika kuhalalisha haramu na kuharamisha halali, kinyume na hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake rehema na Amani zimfikie.
Faida
- Nikuwa kuwatii wanachuoni na wengineo katika viumbe katika kubadili hukumu za Mwenyezi Mungu-ikiwa mwenye kuwatii anajua kuwa huko ni kwenda kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu- ni shirki kubwa.
- Nikuwa kuhalalisha na kuharamisha ni haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Kubainishwa kwa aina miongoni mwa aina za shirki, nayo ni shirki ya kutii.
- Sheria ya kumfundisha mjinga.
- Nikuwa maana ya ibada ni pana, inakusanya yote anayoyapenda Mwenyezi Mungu na kuyaridhia katika maneno na matendo ya wazi na ya siri.
- Kubainishwa upotofu wa wanachuoni na watawa.
- Kuthibitishwa kwa ushirikina wa Mayahudi na Wakristo.
- Nikuwa, asili ya dini ya Mitume ni moja, nayo ni Tauhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu).
- Nikuwa kumtii kiumbe katika kumuasi muumba nikumuabudu.
- Ulazima wa kutaka ufafanuzi kutoka kwa wenye elimu kwa yale ambayo hukumu yake imefichikana.
- Pupa ya maswahaba juu ya elimu.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.